ALIYEKAMATWA KWA TUHUMA ZA UGAIDI KENYA KUFATILIWA TAARIFA ZAKE

Serikali ya Tanzania imesema inafuatilia madai ya mtu anayedaiwa kuwa ni raia wake kukamatwa kwa tuhuma za ugaidi nchini Kenya.

0

Serikali ya Tanzania imesema inafuatilia madai ya mtu anayedaiwa kuwa ni raia wake kukamatwa kwa tuhuma za ugaidi nchini Kenya. Balozi wa Tanzania nchini Kenya, David Simbachawene amesema wanafahamu taarifa za kukamatwa kwa mtu huyo, bado wanafuatilia ili kufahamu kama kweli ni Mtanzania.

Katika tukio hilo watu wawili walikamatwa na maofisa wa Kikosi Maalum na Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi (ATPU), walipokuwa kwenye gari aina ya Toyota Probox yenye namba za usajili KCE 695U, kabla ya kutekeleza shambulio hilo.

Maofisa hao waliwazingira na kuwavamia wawili hao walipokuwa wakizozana na maofisa wa kivuko hicho kuhusu malipo ya kuvusha gari lao.
Wakati wa ukamataji huo, watuhumiwa hao walidaiwa kukutwa na bunduki mbili za AK-47, simu za mkononi pamoja na risasi 150. Mpaka sasa mamlaka za Kenya hazijataja majina ya watuhumiwa hao kwa kile kinachodaiwa kuharibu ushahidi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted