Fahamu kuhusu Taliban, kundi lililochukua siku 10 pekee kuiteka Afghanistan na kumfurusha rais wa nchi

Ilichukua Taliban siku10 pekee kuiteka Afghanistan baada ya kuondoka kwa majeshi ya Amerika na kumlazimsha Rais Ashraf Ghani kutorokea Falme za Kiarabu, ila Taliban ni nani haswa?

0

Ilichukua Taliban siku10 pekee kuiteka Afghanistan baada ya kuondoka kwa majeshi ya Amerika na kumlazimsha Rais Ashraf Ghani kutorokea Falme za Kiarabu, ila Taliban ni nani haswa?

Kundi la Taliban lilizinduliwa mapema miaka ya 1990 kaskazini mwa Pakistan kufuatia kuondoka kwa majeshi ya Usovieti kutoka Afghanistan. JIna Taliban linamaanisha wanafunzi. Azimio la kuundwa kwa Taliban ilikuwa kurudisha amani na usalama na
kuanzisha uongozi wa Sharia mara tu watakapochukua uongozi wa nchi.

Kutoka kusini magharibi mwa Afghanistan, Taliban iliendelea kuteka maeneo mengi na mwaka wa 1995 ikateka wilaya ya Herat inayopakana na Iran, mwaka mmoja baadae Taliban iliteka mji mkuu Kabul na kumpindua Rais Burhanuddin Rabbani, aliyekuwa
mmoja wa waanzilishi wa kundi la Afghan mujahideen lililopinga uvamizi wa Usovieti. Kufikia 1998 Taliban ilikuwa inaongoza 90% ya Afghanistan.

Burhanuddin Rabbani

Waafghan wengi ambao hawakufarahishwa na uongozi wa mujahideen baada ya kuondoka kwa Usovieti walikaribisha uongozi wa Taliban ulioahidi kumaliza ufisadi,kukomesha uasi wa sheria na kujenga miundo msingi.

Mara tu Taliban walipoingia uongozini, waliweka marufuku kutazama televisheni, wasichana waliokuwa na umri wa miaka 10 na zaidi hawakuruhusiwa kuenda shule. Katika tukio lililolaaniwa na mataifa mengi ni kushambuliwa kwa mwanafunzi Malala Yousafzai mwaka wa 2012 alipokuwa akielekea nyumbani kutoka shule.

Kundi la Taliban liligonga vichwa vya habari katika mataifa mengi duniani baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 nchini Amerika. Taliban walituhumiwa kuwapa hifadhi washukiwa wakuu wa mashambulizi hayo, ikiwemo Osama Bin Laden.

Osama Bin Laden

Majeshi ya Amerika yameendeleza vita dhidi ya kundi la Taliban nchini Afghanistan kwa miaka 20, na hatimae baada ya Rais Donald Trump na Taliban kutia saini kwa majeshi hao kundoka Afghanistan ifikiapo 1 Mei majeshi ya Amerika yaliondoka kabla mwishoni mwa mwezi Julai 2021, na kumaliza vita vya miaka mingi nchini humo.

Baada ya kuondoka kwa majeshi ya Amerika, ilichukua Taliban siku 10 pekee kuiteka nchi na kuchukua uongozi. Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani akitorokea Falme za Kiarabu.

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani

Kundi laTaliban limefanya vikao na kutangaza serikali mpya na kuwa taifa hilo ni Emirati ya Kiislamu. Baraza la mawaziri katika serikali mpya linajumuisha wanaume pekee na waliokuwa viongozi wakuu wa Taliban.

Mataifa ya China, Urusi na Pakistan yameendeleza urafiki na Afghanistan.
Hivi maajuzi China iliahidi Afghanistan msaada wa $31 milioni ikiwemo chakula na dozi za chanjo ya UVIKO 19. China imesema ipo tayari kuendeleza mawasiliano na serikali mpya ya Afghanistan.

Wafadhili wameahidi kutoa $1 bilioni kuisadia Afghanistan kupambana na umaskini na njaa ambao umekithiri tangu Taliban walipochukua uongozi na misaada ya kimataifa kupungua.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted