Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za binadamu limetangaza wasanii watakaoshiriki katika tamasha ya Global Citizen Live

Tamasha ya Global Citizen Live hufanyika kwenye siku moja na kuonyeshwa katika mabara yote saba kwa saa 24 kote duniani kupitia televisheni, Apple Music, Apple TV App, YouTube,...

0

Tamasha ya Global Citizen Live hufanyika kwenye siku moja na kuonyeshwa katika mabara yote saba kwa saa 24 kote duniani kupitia televisheni, Apple Music, Apple TV App, YouTube, Twitter na kupitia vituo vya redio katika maeneo tofauti Afrika.

Global Citizen Live ni sehemu moja ya kuleta umoja kati ya mabara saba, na kujaribu kuleta suluhu kwa matatizo yanayokumba nchi zinazoendelea,kama vile ukame, mabadiliko ya tabianchi na upatikanaji wa chanjo dhidi ya UVIKO 19.

Tamasha ya mwaka huu itatumiwa kuyahimiza mataifa tajiri zaidi kutekeleza ahadi zao za kutoa $100 bilioni kila mwaka kushughulikia mahitaji ya hali ya hewa ya nchi zinazoendelea na kuyahimiza mataifa tajiri zaidi duniani ya G7 na mabilionea tofauti duniani kumaliza shida ya njaa kwa kuchangia angalau $6 bilioni ili kusaidia takriban watu milioni 41 walio katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.

Global Citizen live pia itatumika kuhimiza mataifa ya G7 na ya Umoja wa Ulaya kugawa mara moja chanjo bilioni moja za UVIko 19 kwa mataifa ambayo hayana chanjo za kutosha. Tamasha ya Global Citizen mwaka huu itafanyika 25 Septemba, wasanii watakaotumbuiza kutoka Lagos Nigeria ni Tiwa Savage, Davido, Femi Kuti na Made Kuti.

Burna Boy atatumbuiza kutoka jijini New York,Marekani. Msanii Sho Madjozi na Muzi watatumbuiza kutoka mjini Johannesburg,Afrika Kusini na Angelique Kidjo atatumbuiza kutoka mjini Paris,Ufaransa.

Global Citizen ni mchakato mkubwa zaidi duniani wa watu wanaochukua hatua na kujitolea kumaliza umaskini uliokithiri kufikia mwaka 2030. Lengo la Global Citizen ikiwa ni kuleta mabadiliko chanya katika masuala ya uendelevu, usawa, na ubinadamu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted