Msichana wa miaka 15 abakwa mara kadhaa na wanaume 26

Mwaka wa 2020, India ilirekodi visa 28,046 vya ubakaji ikiwa ni takriban visa 77 vya ubakaji kila siku.

0

Mahakama India inachunguza kisa ambapo msichana wa miaka 15 alibakwa mara kadhaa na wanaume tofauti kwa zaidi ya miezi tisa, vituo vya habari vimesema.

Polisi kutoka mji wa Mumbai wanawazuilia watu 26 kwa kuhusika na madai hayo ya ubakaji huo, yaliyoanza Januari. Ripoti kutoka India zinasema kuwa mpenzi wa msichana huyo alirekodi video huku akimbaka. Kisha mvulana huyo na marafiki zake wakatumia video hiyo kumshinikiza kufanya mapenzi nao.

Mamlaka inasema kuwa ubakaji huo uliifanyika katika mitaa tofauti ya Mumbai.Msichana huyo hatimaye aliripoti kisa hicho kwa polisi Jumatano usiku.Kulingana na vituo vya habari,msichana huyo aliwataja takriban wanaume 33 kwa jumla na kuwa aliwajua wanaume wote waliombaka.

Tangu kisa cha 2012 kilichozua ghadhabu kote duniani,ambapo mwanamke mmoja alibakwa na wanaume kadha kwenye basi katika eneo la Nirbhaya ,India imeweka sheria kali za kuwaadhibu wahalifu wa ubakaji.

Mwaka wa 2020, India ilirekodi visa 28,046 vya ubakaji ikiwa ni takriban visa 77 vya ubakaji kila siku.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted