Luteni Kanali Mamady Doumbouya kuapishwa kuwa rais wa mpito Ijumaa 1 Oktoba.

Mamady Doumbouya ataapishwa mwendo wa saa sita majira ya Afrika Magharibi katika ukumbi wa Mohammed V conference centre mji mkuu wa Conakry.

0
Luteni Kanali Mamady Doumbouya

Luteni Kanali Mamady Doumbouya, mwanajeshi aliyeongoza mapinduzi nchini Guinea mwezi Septemba ataapishwa kuwa rais wa mpito Ijumaa 1 Oktoba, mamlaka imesema.

Doumbouya ataapishwa mwendo wa saa sita majira ya Afrika Magharibi katika ukumbi wa Mohammed V conference centre mji mkuu wa Conakry, taarifa kwenye vyombo vya habari imeeleza.

Luteni Kanali Doumbouya atakuwa rais wa mpito, akiongoza kwa muda hadi nchi irudi kwa uongozi wa raia,kulingana na mikakati iliowekwa na junta, ingawaje haikueleza atakuwa rais wa mpito kwa muda gani.

Mapinduzi ya Septemba 5, yalimuondoa uongozini Rais Alpha Conde mwenye umri wa miaka 83. Conde alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia mwaka wa 2010 na baadae kuchaguliwa tena mwaka wa 2015.

Lakini mwaka jana aliunda sheria mpya kwenye katiba ya nchi iliyompa nafasi ya kuwania awamu ya tatu ya urais mwezi Oktoba 2020.

Hatua hiyo ilizua maandamano makubwa ambapo watu wengi waliuawa.Conde alishinda uchaguzi wa 2020 lakini viongozi wa upinzani walipinga ushindi huo.

Alpha Conde, Rais wa Guinea

Mkakati uliozinduliwa Jumatatu unaapa kuwa katiba mpya itaundwa na uchaguzi wa huru, demokrasia na wazi utafanyika, ingawaje haukueleza muda wa mpito utadumu kwa kipindi gani.

Hati inasema kuwa rais wa mpito atakuwa mkuu wa nchi na mkuu wa majeshi na ataamua sera za taifa,na kuwa na nguvu ya kumteua na kumfuta kazi Waziri mkuu wa mpito.

Hata hivyo,rais atazuiwa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi baada ya muda wa mpito.

Msukosuko wa kisiasa nchini Guinea umezua wasiwasi kati ya mataifa jirani na Guinea.

Mapinduzi ya Guinea yalikuwa ya pili katika eneo la Afrika Magharibi baada ya Mali  kwenye kipindi cha miezi 13.

Jumuiya ya ECOWAS inataka uchaguzi ufanyike kwenye miezi sita na kuachiwa kwa Conde.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted