Fahamu wafungwa wengine waliofaulu kutoroka kutoka magereza yenye ulinzi mkali zaidi duniani

Watuhumiwa watatu wa ugaidi Musharaf Abdalla almaarufu Alex Shikanda, Joseph Juma Odhiambo, na Mohammed Ali Abikar walitoroka kutoka gereza la Kamiti mnamo Jumatatu, Novemba 15. Wafungwa hao watatu...

0

Watuhumiwa watatu wa ugaidi Musharaf Abdalla almaarufu Alex Shikanda, Joseph Juma Odhiambo, na Mohammed Ali Abikar walitoroka kutoka gereza la Kamiti mnamo Jumatatu, Novemba 15.

Wafungwa hao watatu wa ugaidi, ambao siku ya Jumapili walitoroka kutoka kwa gereza la Kamiti walikamatwa katika msitu wa Enzio huko Mwingi Mashariki katika Kaunti ya Kitui. Watatu hao walikamatwa kufuatia taarifa kutoka kwa umma na inaaminika walikuwa wakielekea Somalia.

Watuhumiwa hao walinaswa baada ya kusimama kununua maji, maziwa na biskuti. Mmoja wa wafungwa aliwaambia polisi na wenyeji waliowakamata kuwa wangewahonga iwapo wangekuwa na simu za rununu.

Watuhumiwa 3 wa ugaidi Musharaf Abdalla,Joseph Juma Odhiambo, na Mohammed Ali

Mnamo Jumamosi 20 Novemba, maafisa watatu walikamatwa na msako kuanzishwa baada ya washukiwa watatu kutoroka kutoka kizuizini katika Kituo cha Polisi cha Kilgoris.

Watuhumiwa hao Shadrack Leparan, Enock Ndege na Patrick Mausa, walitoroka kupitia shimo walilotengeneza baada ya kutoa matofali kutoka kwenye ukuta wa seli yao, inasemekana walikimbia kuelekea kitongoji cha Kilgoris.

Shadrack Leparan (29) alikuwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za mauaji huku Enock Ndege (28) akiwa jela kwa wizi. Kulingana na ripoti  watatu hao walikuwa miongoni mwa washukiwa watano waliokuwa wakishikiliwa katika seli. Afisa wa zamu ya usiku, Koplo Carlmax Okello, pia alisema hakusikia washukiwa wakitoroka.

Kando na wafungwa hawa kutoka Kenya ambao wamefaulu kutoroka jela yenye ulinzi mkali ya Kamiti, wapo wafungwa wengine kwenye historia waliofaulu kutoroka kutoka magereza yenye ulinzi mkali hata zaidi.

Ted Bundy

Mbakaji na muuaji kutoka Amerika Ted Bundy alifaulu kutoroka kutoka gerezani mara mbili. Mara ya kwanza aliruka kutoka dirisha la ghorofa ya pili ya jela alikokuwa amezuiliwa,alikamatwa baada ya siku sita.

Mara ya pili, Ted Bundy alifanikiwa kupenyeza kwenye tundu kwenye seli yake hadi kwenye ghorofa ya mkuu wa gereza. Kutoka hapo, alifika juu ya jengo hilo na kuvuka hadi eneo lingine la kituo hicho. Huko alikuta nguo za mlinzi wa nyumba alizivaa na akafaulu kutoka nje kupitia mlango wa mbele wa gereza.

Hakuna aliyejua kwamba alikuwa ametoroka kwa saa kumi na saba, na wakati huo, Bundy alikuwa upande mwingine wa nchi. Ted Bundy alikamatwa tena na kupatikana na hatia kwa makosa 36 ya mauaji na kuhukumiwa kifo.

Ted Bundy

Gereza la Alcatraz lililoko katikati mwa mwamba katika Ghuba ya San Francisco ililionekana kuwa mojawapo ya magereza yenye ulinzi mkali zaidi nchini Amerika kwa wakati huo na haikuwa rahisi kwa wafungwa kutoroka kutoka gereza hilo la kisiwani.

Mnamo mwaka wa 1962, Frank Morris na kaka zake John na Clarence Anglin waliokuwa na historia ndefu ya majaribio kadhaa ya kutoroka jela,walifungwa wote kwenye gereza la Alcatraz. Halikuwa swali la “ikiwa” wangejaribu kutoroka, ila “lini”.  Hatimaye, kwa usaidizi wa vijiko vilivyoimarishwa na visu walipanua shimo la uingizaji hewa katika seli zao na kupenyeza.

Huenda walifaulu kutoroka na kubadili majina yao au walizama baharini au labda waliliwa na papa. Kulingana na FBI, walikubali kuwa mbinu yao ya kutoroka ilikuwa ya ujanja, ukurasa wa tovuti ya ofisi hiyo kuhusu kesi hiyo bado ulikuwa unaomba taarifa za umma kuhusu watu hao watatu.

Gereza la Alcatraz

JOAQUIN ‘EL CHAPO’ GUZMAN

Mlanguzi wa dawa za kulevya wa Mexico anayeitwa El Chapo alifaulu kutoroka mara mbili kutoka magereza ya Mexico yenye ulinzi mkali.

Mnamo Januari 2001, mlinzi wa gereza alifungua mlango wa seli ya kielektroniki ya Guzmán huku mtu aliyesukuma kontena la nguo lililojaa nguo chafu akipita mbele ya seli ya El Chapo, El Chapo aliingia kwenye kontena hiyo na kisha akaingizwa kwenye lori lililombeba mlanguzi huyo wa dawa za kulevya kutoka gerezani. Uchunguzi ulibaini kuwa takriban watu sabini na wanane walihusika katika kumtorosha ElChapo na ilimgharimu takriban dola milioni 2.5. Alikwepa kukamatwa tena kwa miaka 13 mingine.

JOAQUIN ‘EL CHAPO’ GUZMAN

Mnamo 2014, kiongozi huyo wa walanguzi wa dawa za kulevya kutoka jimbo la Sinaloa Mexico, baada ya kukamatwa tena alifaulu kutoroka tena jela. El Chapo hakutoroka gerezani tu, bali aliendesha pikipiki kupitia mtaro uliokuwa umechimbwa kutoka kwenye seli yake hadi nje.

Baada ya miezi kadhaa ya kukimbia – na mahojiano na mwigizaji wa Hollywood Sean Penn – Guzman hatimaye alikamatwa tena katika jimbo la Sinaloa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted