Umoja wa mataifa kuhamisha familia za wafanyakazi wake kutoka Ethiopia

Agizo hilo lilitolewa baada ya Ufaransa kuwa nchi ya hivi punde kuwashauri raia wake kuondoka Ethiopia, kufuatia ushauri sawa na wa Amerika na Uingereza

0

Umoja wa Mataifa utahamisha familia wa wafanyakazi wake wanaofanya kazi nchini Ethiopia,hayo ni  kulingana na waraka rasmi wa UN, huku waasi wakidai kuelekea mji mkuu Khartoum.

Amri ya usalama ya Umoja wa Mataifa imelitaka shirika hilo “kuratibu uhamishaji na kuhakikisha kuwa familia zote wastahiki wanaondoka Ethiopia kabla tarehe 25 Novemba 2021.”

Agizo hilo lilitolewa baada ya Ufaransa kuwa nchi ya hivi punde zaidi kuwashauri raia wake kuondoka Ethiopia, kufuatia ushauri sawa na wa Amerika na Uingereza katika wiki za hivi karibuni wakati mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Tigray yakikaribia Addis Ababa.

“Raia wote wa Ufaransa wanahimizwa kuondoka nchini bila kuchelewa,” Ubalozi  wa Ufaransa mjini Addis Ababa ulisema katika barua pepe iliyotumwa kwa raia wa Ufaransa.

Wafanyikazi wa ubalozi walikuwa wakichukua hatua kuwaondoka raia wake kwa kuhifadhi viti kwenye ndege za kibiashara na “ikiwezekana”wangepanga safari ya kukodi, barua pepe hiyo ilisema.

Ethiopia kaskazini imekumbwa na mzozo tangu Novemba 2020 wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipotuma wanajeshi katika eneo la Tigray kupindua chama chake tawala cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2019 aliahidi ushindi wa haraka, lakini kufikia mwishoni mwa Juni TPLF ilikuwa imejipanga upya na kutwaa tena sehemu kubwa ya Tigray ikiwa ni pamoja na mji mkuu wake wa kikanda Mekele.

Abiy Ahmed, Waziri mkuu Ethiopia

Tangu wakati huo TPLF imeingia katika mikoa jirani ya Afar na Amhara na wiki hii ilidai udhibiti wa Shewa Robit, kilomita 220 tu (maili 135) kaskazini mashariki mwa Addis Ababa.

Baadhi ya wapiganaji wa TPLF waliaminika kufika Debre Sina, takriban kilomita 30 karibu na Addis Ababa, wanadiplomasia waliofahamishwa kuhusu hali ya usalama walisema. Kukatika kwa mawasiliano katika sehemu kubwa ya eneo lililokumbwa na migogoro kumefanya hakli halisi ya mapigano kuwa ngumu kuthibitisha.

Serikali haijajibu masuali kuhusu hali ya Shewa Robit.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika katika Pembe ya Afrika, Olusegun Obasanjo, anaongoza msukumo mkali wa kutaka kusitishwa kwa mapigano, lakini hadi sasa kumekuwa na mabadiliko machache.

Siku ya Jumatatu Abiy alionekana kutilia shaka matarajio ya suluhu la amani, akitangaza kuwa anaelekea mstari wa mbele kuongoza vikosi vya ulinzi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted