Watu saba wamefariki kwa kula samaki mwenye sumu

Watu 7 wamefariki dunia na wengine 24 kulazwa katika Hospitali ya Wilaya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kula kitoweo cha samaki aina ya kasa anayedaiwa kuwa...

0

Watu saba wamefariki dunia na wengine 24 kulazwa katika Hospitali ya Wilaya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kula kitoweo cha samaki aina ya kasa anayedaiwa kuwa na sumu.

Tukio hilo lilitokea Novemba 25,2021 eneo la Soko la Msuka na Tumbe katika wilaya ya Micheweni ambapo inadaiwa kuwa watu hao mara baada ya kula samaki huyo walianza kutapika na kuharisha ndipo walipopelekwa hospitalini.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Juma Sadi Khamis amesema siiku hiyo walikufa watu watatu, tarehe 27 wakafa wengine wawili na na jana Jumapili wamefariki  wengine wawili, hivyo kufikia idadi ya watu saba waliofariki dunia kutokana na tukio hilo.

Aidha ameongeza kuwa watu 16 kati ya 24 waliokuwa wamelazwa wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya afya zao kuimarika huku wengine wanane wakiendelea kupata matibabu.

“Huyo samaki yeye mwenyewe anasumu kama ukimkosea kumpika bila kuondoa sumu yote lakini pia inawezekana walimtoa sumu ila kutokana na samaki hao kutoweka duniani kwahiyo kuna baadhi ya mataifa wanawadunga sindano za sumu wanapowafuga ili wasiliwe,” amesema na kuongeza

“Kwahiyo inawezekana hata huyo alikuwa anafugwa sehemu sasa akaja kwenye ukanda huu wa kwetu wakamkamata na kumfanya kitoweo bila kujua kama ana sumu,”

Kasa ni viumbe amabo wapo katika kundi la Reptilian ametajwa kuwa ndio kiumbe mwenye kumbukumbu kubwa katika kundi lake. Kasa hutaga mayai 7000 katika maisha yake na kwa kila msimu Kasa mmoja anaweza kuwa na viota vinne mpaka sita ambapo huwa na mayai 80 mpaka 180.Kasa ni kivutio kizuri kwa watalii ambao hupenda kutembelea maeneo ya fukwe kama vile hifadhi ya taifa Saadani ambako viota vya kasa hupatikana.

Kasa ni viashiria vya biolojia kwa huonyesha hali ya mazingira hasa ya majini na vilevile hutumika katika shughuli za utafiti na kujifunza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted