Kirusi kipya cha UVIKO 19,Omicron kilikuwepo Ulaya hata kabla Afrika Kusini kuripoti kisa cha kwanza

Kirusi kipya Omicron kilikuwepo Ulaya kabla kisa cha kwanza kuripotiwa Afrika Kusini, data mpya imethibitisha

0

Kirusi kipya cha UVIKO 19 Omicron kilikuwepo Ulaya kabla kisa cha kwanza kuripotiwa nchini Afrika Kusini, data mpya kutoka Uholanzi ilionyesha Jumanne, huku Amerika ya Kusini ikiripoti visa vyake viwili vya kwanza nchini Brazil.

Katika wiki ya kwanza tangu aina mpya ya kirusi kuripotiwa kwa Shirika la Afya Ulimwenguni na Afrika Kusini, mataifa kadhaa yamekimbilia kuweka vizuizi vya kusafiri, huku vizuizi vingi vikilenga mataifa ya kusini mwa Afrika.

Lakini Shirika la Afya Ulimwenguni lilionya Jumanne — huku Canada ikipanua vikwazo vyake na kujumuisha mataifa ya Misri na Nigeria — kwamba marufuku hizo usafiri zitaleta madhara kuliko mema.

Ubatili wa vizuizi vya kusafiri ulisisitizwa baada ya viongozi wa Uholanzi kuripoti kuwa kirsui cha Omicron kilikuwepo nchini humo kabla ya Afrika Kusini kuripoti kisa chake cha kwanza, mnamo Novemba 25.

Shirika la Afya Duniani (WHO) inaamini kuwa kirusi cha Omicron kinaweza kuambukiza kwa haraka na ni sugu kwa chanjo. Kabla Afrika Kusini kuripoti kisa cha kwanza, Omicron ilikuwa imepatikana katika sampuli mbili zilizofanyiwa utafiti nchini Uholanzi kati ya Novemba 19 na 23.

Kwa kuwa nchi nyingi sasa zinawasiwasi kuhusu kirusi kipya cha Omicron, ni wazi kuwa kirusi hicho kimekuwa kikienea wapi na kwa muda gani. Kufikia sasa, nchi nyingi zimegundua kuwepo kwa kirsui hicho ikijumuisha Australia, Uingereza, Canada, Hong Kong, Israel, Italia na Ureno.

Miongoni mwa nchi za Ulaya, Ubelgiji na Ujerumani zote zimeripoti visa viwili vya aina hiyo mpya ya UVIKO 19 kabla tarehe Novemba 25 wakati Afrika Kusini iliripoti kisa chake cha kwanza,Visa hivyo vikiripotiwa miongoni mwa wasafiri.

Amerika ya Kusini iliripoti visa viwili vya kwanza Jumanne kati ya watu waliosafiri kutoka Afrika Kusini kwenda Brazil. Kisa cha kwanza kilithibitishwa huko Japan, siku moja baada ya kuwaweka marufuku kwa wasafiri wote wa kigeni.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted