Wananchi wa Gambia hutumia gololi badala ya karatasi kupiga kura.

Mfumo huu unategemea matumizi ya gololi ambazo hutumbukizwa kwenye debe lillilotengenezwa kwa chuma

0
Gololi za kupigia kura

Gambia inaendesha uchaguzi wake kupitia mfumo wa kipekee wa upigaji kura ambao ulianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1960 ili kukabiliana na viwango vya juu vya watu wasiojua kusoma na kuandika nchini humo.

Mfumo huu unategemea matumizi ya gololi ambazo hutumbukizwa kwenye debe lililotengenezwa kwa chuma. Kila mgombea huwa na debe lake ambalo hupakwa rangi za chama chake au kubandikwa picha yake na wafuasi wake hutumbukiza gololi hizo wanapompigia kura.

Siku ya uchaguzi, katika kituo cha kupigia kura, hilo hilo huwekwa nyuma ya kibanda cha kupigia kura. Wapiga kura, baada ya kupewa gololi huenda hadi kwenye chumba cha kupigia kura ili kupiga kura.

Wakati gololi inapopenyezwa kwenye debe la chama/mgombea aliyechaguliwa, na kuanguka, hugonga kengele ambayo mlio wake huashiria wazi kwa watazamaji katika kituo cha kupigia kura kwamba kura imepigwa.

madebe ya kupigia kura

Ili kuzuia kusikia sauti nyingine, wanapofunga debe maafisa wa kupiga kura huweka mchanga. Inafurahisha pia kuangazia kwamba, kwa kuwa mlio wa kengele ni kama wa kengele ya baiskeli, siku ya uchaguzi baiskeli hupigwa marufuku kufika maeneo ya kupigia kura.

Shughuli ya kupiga kura inapokamilika, gololi hutolewa na kuwekwa kwenye trei maalum (zenye matundu 200 au 500), mfumo rahisi unaoruhusu maafisa wa kuhesabu kura kufahamu haraka idadi ya kura zilizopigwa katika kila debe.

Faida kuu na dhahiri ya mfumo huu wa kipekee wa upigaji kura ni kwamba ni rahisi na ni bei nafuu. Wapiga kura wa Gambia wanauelewa vyema mfumo huo na inasemekana ni vigumu kuiba kuiba kura.

Kadiri wagombea wanavyoshindana katika uchaguzi, ndivyo vyumba vya kupigia kura vinapaswa kuwa vikubwa. Iwapo kengele itakosa kutoa mlia wakati mpiga kura yuko ndani ya chumba cha kupigia kura, maafisa wa upigaji kura wanatakiwa kuangalia kama gololi imepenyezwa vibaya na mpiga kura.

Mojawapo ya hasara za mfumo huu ni kwamba hauruhusu wapiga kura kutopiga kura bila kumchagua mgombea yeyote.

Kutokuwepo kwa mlio kunaonyesha wazi kwa hadhira katika kituo cha kupigia kura kwamba kura haikupigwa katika moja wapo ya madebe hayo.

Zaidi ya hayo, iwapo kutatokea mizozo inayohusiana na uchaguzi, kukosekana kwa karatasi za kupigia kura hufanya kuhesabiwa upya kwa kura baada ya uchaguzi kuwa zoezi ambalo linaweza kuwa gumu zaidi kufuta au kukataa.

Hata hivyo, mfumo huu wa kupiga kura unasalia kuwa mfumo rahisi sana wa kupiga kura katika nchi yenye idadi kubwa ya wapiga kura wasiojua kusoma na kuandika na yenye rasilimali chache za kifedha.

Juhudi za elimu kwa wapiga kura zinaweza kuwasilishwa  kwa urahisi ili kuwapa wapiga kura maelezo ya kimsingi kuhusu jinsi ya kutambulisha gololi kwenye debe la rangi ya chama.

Kwa kuhitimisha; kama juhudi za kuunga mkono mchakato wa uchaguzi nchini Gambia, Taiwan ilitoa takriban gololi milioni 1.5 ili zitumike kama kifaa cha kupigia kura.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted