Raia wa Korea Kaskazini wamepigwa marufuku kucheka au kunywa pombe wakiadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Kim Jong Il.

“Hata kama jamaa yako ataaga dunia wakati wa maombolezo, huruhusiwi kulia kwa sauti ya juu. Watu hawawezi hata kusherehekea siku zao za kuzaliwa ikiwa siku hiyo itakuwa ndani...

0
Kim Jong il, kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini

Raia wa Korea Kaskazini wamepigwa marufuku kucheka au kunywa pombe kwa siku 11 wakiadhimisha miaka kumi tangu kifo cha kiongozi wa zamani Kim Jong Il.

Mamlaka za serikali zimeamuru umma kutoonyesha dalili zozote za furaha wakati Korea Kaskazini ikiadhimisha kifo chake.

Kim Jong Il alitawala Korea Kaskazini kuanzia 1994 hadi kifo chake mwaka 2011, kisha akarithiwa na mwanawe wa tatu amabye ndio kiongozi wa sasa Kim Jong Un.

Miaka kumi sasa baada ya kifo chake, Wakorea Kaskazini wanalazimika kuadhimisha muda wa siku 11 wa maombolezo ambapo hawaruhusiwi kucheka wala kunywa pombe.

“Wakati wa maombolezo, hatupaswi kunywa pombe, kucheka au kuwa na burudani,” Mkorea Kaskazini kutoka mji wa mpaka wa kaskazini-mashariki wa Sinuiju aliiambia Radio Free Asia

Chanzo hicho kiliongeza kuwa Wakorea Kaskazini hawaruhusiwi kwenda madukani mnamo Desemba 17 siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kim Jong Il.

Waliongeza kuwa “zamani watu wengi ambao walikamatwa wakinywa pombe au kulewa wakati wa maombolezo walikamatwa na kuchukuliwa kama wahalifu wa kiitikadi. Walikamatwa na hawakuonekana tena.”

“Hata kama jamaa yako ataaga dunia wakati wa maombolezo, huruhusiwi kulia kwa sauti ya juu. Watu hawawezi hata kusherehekea siku zao za kuzaliwa ikiwa siku hiyo itakuwa ndani ya kipindi cha maombolezo.”

Kim Jong Il alifariki baada ya kupata mshtuko wa moyo mnamo Desemba 17 2011 akiwa na umri wa miaka 69 baada ya kutawala nchi hiyo kwa miaka 17.

Kipindi cha maombolezo hufanyika kila mwaka kwamuda wa siku 10, mwaka huu kipindi hicho kimeongezwa hadi siku 11 kuadhimisha miaka kumi baada ya kifo chake.

Chanzo kingine, mkazi wa jimbo la kusini-magharibi mwa Hwanghae Kusini, alisema maafisa wa polisi waliambiwa waangalie watu ambao wanashindwa kuonekana wamehuzunika ipasavyo wakati wa maombolezo.

Chanzo hicho pia kiliongeza kuwa vikundi vya wananchi na makampuni yanayomilikiwa na serikali yameagizwa kuwatunza watu maskini katika kipindi cha maombolezo, wakati nchi ikikabiliwa na tatizo la chakula.

Mkazi huyo ambaye jina lake halikutajwa aliongeza kuwa maombolezo ya Kim Jong Il, na babake Kim Il Sung, yanaathiri maisha ya kila siku ya Wakorea Kaskazini.

Walisema: “Natumai tu kwamba muda wa maombolezo ya Kim Jong Il utafupishwa hadi wiki moja, kama vile kipindi cha maombolezo ya Kim Il Sung.

“Wakazi wanalalamika kwamba walio hai wanalazimika kuomboleza watu hawa wawili waliokufa.”

Vizazi vitatu vya familia ya Kim vimetawala Korea Kaskazini tangu Kim Il Sung alipoanzisha nchi hiyo mwaka 1948. Kim Il Sung alipofariki mwaka 1994, mwanawe mkubwa, Kim Jong Il, alirithi madaraka.

Kim Jong Un ni mtoto wa tatu na mdogo wa kiume wa Kim Jong Il na alichukua mamlaka baada ya kifo cha babake mwaka wa 2011.

Ili kuadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi ya kifo cha Kim Jong Il, majimbo mbalimbali kote Korea Kaskazini yanafanya maonyesho ya picha zake na kufanya matamasha kwa kumbukumbu yake.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted