Tanzania: Watu 3,147 waliugua corona mwaka jana

Kati ya watu hao 2990 walikuwa hawajachanja chanjo ya ugonjwa huo.

0
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Wizara ya Afya nchini Tanzania, imesema kati ya Septemba 2021 mpaka Januari 23, 2022, watu 3147 walilazwa hospitalini kutokana na Uviko-19 ambapo kati yao 2990 sawa na asilimia 95 walikuwa hawajachanja.

Pia, imesema kuwa mpaka sasa ni watu 1,922,019 waliochanja sawa na asilimia 3.3 ya Watanzania waliolengwa.

Waziri wa Afya nchini humo Ummy Mwalimu, ameayazungumza hayo hii leo mara baada ya  kupokea shehena ya chanjo 800,000 za Sinopharm ambazo ni sawa na dozi 400,000 kutoka Serikali ya watu wa China.

Ummy ameongeza kuwa kwa siku ya Januari 23,2022 pekee  kulikuwa na watu 31 waliolazwa ICU, lakini kati ya hao 30 walikuwa hawajachanjwa.

“Wagonjwa waliokuwa mahututi katika vyumba vya uangalizi maalumu kwa siku ya Januari 23 mwaka huu ICU walikuwa 31 kati yao 30 walikuwa hawajachanjwa.

Aidha Ummy amesema katika jumla ya wagonjwa wote waliolazwa katika kipindi hicho jumla ya vifo 76 vilitokea huku 73 viliwahusisha wagonjwa ambao hawakuchanja.

Aidha amewataka Watanzania kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima kwa kuwa si kila homa au mafua ni Uviko-19.

“Una homa kapime watu sasa hivi wanakunywa Azuma na dawa zingine za antibaotiki, si kila homa ni corona tuache kujitibu kapime upate matibabu sahihi, tunatengeneza usugu wa dawa baadaye tutakua tunatibu watu hawaponi,” amesema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted