Kesi ya Mbatia yagonga mwamba

Kesi hiyo aliyoifungua kupinga utaratibu wa kujiuzulu Spika Ndugai imegonga mwamba baada ya Mahakama kuitupilia mbali

0

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam leo imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akipinga utaratibu wa kujiuzulu aliotumia aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Nduga

Mbatia ambaye anawakilishwa na jopo la mawakili saba wa watoa maombi wakiongozwa na Daimu Halfan alifungua kesi ya kikatiba inayohusiana na ukiukwaji wa katiba uliofanywa wakati Job Ndugai akijiuzulu kwenye nafasi ya Spika wa Bunge.

Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji John Mgeta ambapo wamesema Ndugai alifuata utaratibu kwa kuwa aliwasilisha barua kwa mujibu wa ibara ndogo (1) (2) hakuna na shaka kwamba ibara hiyo inatoa taratibu ambazo Spika akitaka kujiuzulu lazima azifuate.

Jaji Mgeta amesema Bunge ni taasisi yenye maofisa wenye wajibu wa kutekeleza shughuli za kila siku moja ya maofisa hao ni Katibu wa Bunge.

“Kwa mujibu wa ibara ya 149 kifungu kidogo cha 2 imetajwa katibu kwamba notice ya kujiuzulu inaweza kuwasilisha kwake, kama Ndugai alikuwa na nia ya kujiuzulu Bunge siku hiyo halikukaa kikao je Ndugai angewasilisha wapi notice yake,” amesema Mgeta

Aidha amesema kwa mujibu wa ibara hiyo hiyo aliyetajwa ni katibu ndiye na aliyepokea barua siku hiyo na nakala ya kujiuzulu iliwasilishwa kwa mtu sahihi 

“Ndiyo maana katibu wa bunge aliitisha kikao cha Bunge kwa wabunge hivyo amebaini shauri la Mbatia halina msingi linatupwa na kila upande wajigharamie wenyewe.

Awali jopo la mawakili saba wa wajibu maombi ikiongozwa na wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata waliweka pingamizi wakidai Mbatia alitakiwa kuweka kiapo kinachothibitisha namna mtu alivyoathirika na ukiukwaji ukoje.

Mlata amedai kuwa watoa maombi walipaswa waweke kiapo kinachothibitisha jinsi ngani mtu huyo ameathirika na ukiukwaji ukoje.

Amedai kuwa walipaswa waeleze hakuna njia nyingine ya kushughulikia hayo madai isipokuwa kuleta shauri kwa njia ya kikatiba.

Pia amedai watoa maombi walitakiwa watumie njia nyingine walipaswa kuitumia katika kuleta malalamiko hayo mahakamani.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted