IGP Sirro:Tukio Mtwara lisiwafanye Watanzania kutoliamini jeshi lenu

Asema hata kama ni Askari atashghulikiwa kama wahalifu wengine, na yeye hawezi kulinda mtu wa hovyo hovyo

0
IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro, amewaambia wananchi kuwa tukio la Mtwara lililowahusisha Maofisa wa Jeshi la Polisi, kumuua kijana Mussa Hamis na kisha kumnyanganya shilingi milioni 33.7, lisiwafanye Watanzania kutoliamini jeshi lao. 

IGP Sirro ameyasema hayo akiwa jijini Tanga katika wilaya ya Kilindi, wakati wa mkutano na wananchi wa eneo hilo ambapo hivi karibuni kulitokea mauaji ya watu sita yalihusisha wakulima na wafugaji.

Sirro amesema kuwa hakuna aliyejuu ya sheria katika matukio ya uhalifu haijalishi mtu huyo yupo na cheo gani isipokuwa sheria itafata mkondo wake, huku akigusia Maofisa saba wa Jeshi la polisi wanaotuhumiwa kumuua kijana Mussa.

“Limetokea tukio la Mtwara, kuna maofisa na askari wa hovyo hovyo wamefanya tukio la hovyo hovyo mimi siwezi kulinda mtu wa hovyo hovyo, hata kama ni askari, hata kama ni ofisa ukifanya mambo ya hovyo hovyo, ukijingiza kwenye ujambazi, ukijiingiza kwenye mambo ya rushwa utashughulikiwa kama mhalifu mwinmgine.” amesema IGP Sirro.

Aidha IGP Sirro, ametoa onyo kwa wale wote wanaoendelea ama wanaotaka kufanya uhalifu nchini kuwa Jeshi la Polisi, litashughulika na wahalifu wote popote pale walipo huku akisisitiza, kuwa jeshi hilo halimuoenei mtu hivyo wananchi wametakiwa kusaidia kutoa taarifa zenye viashiria vya uhalifu.

“Hakuna tukio la kihalifu linaloweza kufanyika nchi hii tusiweze kuwakamata wahusika, na bahati nzuri raia wema wanatusaidia sana kutoa taarifa”.amesema IGP Sirro.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted