Waasi 33 wauawa mashariki mwa DR Congo

Makundi ya waasi ya FNL na RED-Tabara yana kambi mashariki mwa DR Congo, eneo ambalo limevurugika kutokana na kuwepo kwa makundi mengi yenye silaha ndani na nje ya...

0

.Jeshi la Congo lilisema Ijumaa kuwa wanajeshi wake waliwauwa watu 33 wenye silaha katika mapigano dhidi ya wanamgambo wa ndani wanaoshirikiana na waasi wa Burundi mashariki mwa DR Congo.

Operesheni hiyo kubwa ilitekelezwa kuanzia Jumatano hadi Alhamisi katika jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jeshi hilo lilikuwa likipambana na wanamgambo wa Mai-Mai, ambao ni washirika wa FNL ya Burundi (National Forces of Liberation) na waasi wa RED-Tabara.

Msemaji wa jeshi la mkoa Luteni Marc Elonga Kyondwa alisema waliouawa katika  mapigano hayo ni “wanamgambo 33, wakiwemo viongozi watatu.”

“Hili lilikuwa ni jibu la jeshi dhidi ya makundi haya ya waasi wanaoendesha shughuli zao kwenye milima inayotazamana na mji wa Uvira” baada ya shambulio kwenye moja ya vituo vyake, msemaji huyo aliliambia shirika la habari la AFP, akiongeza kuwa wanajeshi sasa wanadhibiti eneo hilo huku operesheni za kuwaondoa zikiendelea.

Makundi ya waasi ya FNL na RED-Tabara yana kambi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo limevurugika kutokana na kuwepo kwa makundi mengi yenye silaha ndani na nje ya nchi.

Jeshi la Congo mara kwa mara linawashutumu waasi wa Burundi kwa kushirikiana na wanamgambo wa ndani na kusababisha ukosefu wa usalama katika jimbo la Kivu Kusini.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted