Mauzo ya bidhaa za Tanzania na Rwanda yafikia Dola milioni 269.

Tanzania na Rwanda zilitia saini mkataba wa kukuza biashara ya mipakani na kuwakaribisha wafanyabiashara kushiriki katika kamati ya pamoja ya mpaka.

0

Imeelezwa kuwa biashara kati ya Tanzania na Rwanda hivi sasa imefikia Dola za Marekani milioni 274.6 ambazo sawa na takribani shilingi  bilioni 635 za Tanzania,  huku nchi hizo zikitakiwa kukabiliana na vikwazo vilivyopo ili kuimarisha usafirishaji huru wa bidhaa na mwingiliano wa watu kati ya nchi hizo.

Kwa mujibu wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa, mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenda Rwanda yamefikia Dola milioni 269.6 wakati mauzo ya Rwanda kwenda Tanzania yamefikia Dola milioni 5.

Mtaalamu wa Sera kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda Rwanda, James Tayebwa, alisema Tanzania na Rwanda zilitia saini mkataba wa kukuza biashara ya mipakani na kuwakaribisha wafanyabiashara kushiriki katika kamati ya pamoja ya mpaka ili kujadili na kuunda mpango madhubuti wa utekelezaji wa makubaliano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara ya Afrika Mashariki (EABC), John Bosco alisema kabla ya Covid-19, Kituo cha Mpakani cha Rusumo kilikuwa kinasafirisha malori 400 kila siku.

Kituo cha Mpakani cha Rusumo kinachounganisha Rwanda na Tanzania pia ni lango muhimu kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo pia inatarajia kuwa mwanachama wa EAC.

Itifaki ya Soko la Pamoja la EAC ilitiwa saini na wakuu wa nchi tano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Novemba 20, 2009 ili kuhakikisha usafirishaji huru wa bidhaa, watu, huduma, vibarua na mitaji, matumizi ya sarafu moja kwa shughuli za kila siku ndani ya Soko la Pamoja, shirikisho la kisiasa pamoja na umoja wa forodha.

Lengo kuu la Itifaki ya Soko la Pamoja ni kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kukuza uhusiano wa kijamii wa raia wa Afrika Mashariki kupitia kuondoa vizuizi vya biashara ya kikanda na harakati za raia wa Afrika Mashariki.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted