Mke wa Ali Kiba adai talaka

“Mlalamikiwa (Ali Kiba) amefanya mzaha kwa ndoa yetu kwa kujihusisha bila heshima katika maonyesho ya hadharani ya uzinzi na wanawake mbalimbali bila kujali kabisa hisia za mlalamishi,” Khalef...

0
Ali Kiba na mkewe Amina Khalef

Mwanamuziki wa Tanzania, Ali Salehe Kiba huenda akapata talaka kutoka kwa mkewe Mkenya Amina Khalef.

Msanii huyo wa Bongofleva alifunga ndoa na Amina Khalef mjini Mombasa 2018. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wengi mashuhuri kutoka Kenya na Tanzania akiwemo gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.

Ali Kiba anashtakiwa kwa kuacha ndoa yake na amepewa wiki mbili kujibu madai hayo.

Amina Khalef amemshutumu nyota huyo wa Bongoflava anayetajwa kuwa miongoni mwa wanamuziki maarufu Afrika Mashariki kwa kumtusi na kuwa amekosa kuwa mwaminifu kwake.

“Iwapo utakosa kufika mahakamani ndani ya muda uliotajwa, mlalamishi anaweza kuendelea na kesi na hukumu kutolewa bila wewe kuwepo”, amri katika mahakama ya Kadhi Mombasa ilisema.

“Mlalamikiwa (Ali Kiba) amefanya mzaha kwa ndoa yetu kwa kujihusisha bila heshima katika maonyesho ya hadharani ya uzinzi na wanawake mbalimbali bila kujali kabisa hisia za mlalamishi,” Khalef anasema katika karatasi za mahakama.

Pia amemshutumu mwimbaji huyo kwa kushindwa kukidhi mahitaji ya familia, ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi na ameomba msaada wa kila mwezi wa KSh200,000 na matibabu kwa watoto wao wawili.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted