Uchunguzi kufanyika chanzo cha ndege kupata ajali Comoro.

Ndege hiyo ilipata ajali ikiwa chini ya kampuni ya Airline AB Aviation ya Comoro, baada ya kuikodisha kutoka kampuni ya Fly Zanzibar na ilikuwa imeshatimiza takribani wiki moja...

0

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania (TCAA), imesema itachukua hatua za kisheria iwapo itabaini kuna makosa ya kibinadamu, yaliyosababisha ajali ya ndege nchini Comoro.

Mnamo siku ya Jumapili ya Februari 27 zilisambaa taarifa kuwa, ndege ndogo aina ya Cessna Caravan 5HMZA ikiwa na abiria 14 wakiwamo marubani wawili wa Tanzania ilipotea katika rada kilometa 2.5 kabla ya kutua katika mji wa Fomboni, uliopo kisiwa cha Moheli ikitokea makao makuu ya kisiwa cha Moroni.

Ndege hiyo ilipata ajali ikiwa chini ya kampuni ya Airline AB Aviation ya Comoro, baada ya kuikodisha kutoka kampuni ya Fly Zanzibar na ilikuwa imeshatimiza takribani wiki moja tangu ianze kazi huko.

Mmiliki wa kampuni ya Fly Zanzibar Limited, Mazrui Mohammed, alidai sababu za ajali ni mabadiliko ya hali ya hewa visiwani humo.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alisema kuwa mamlaka kwa kushirikiana na mamlaka ya anga nchini Comoro inafanya uchunguzi, lakini pia itatuma wataalam kutoka TCAA watakaokwenda kutoa ushirikiano 

Aidha amesema kama kuna makosa hatua za kisehria zitachukuliwa huku akibainisha kuwa ajali za ndege ni mara chache sana kutokea.

Hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa miongoni mwa waliokuwa kwenye ndege hiyo ni ndugu wa mmiliki wa kampuni ya Fly Zanzibar Limited, Mazrui Mohammed.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) limenukuu taarifa za Serikali ya Comoro ikisema abiria 12 kati wa 14 waliopotea kwenye ndege hiyo walikuwa ni raia wa Comoro na wawili ambao ni marubani ni raia wa Tanzania.

Marubani waliopotea katika ajali hiyo ni Adili Sultani na Ashraf Abdallah Juma ambao amekuwa marubani wa ndege hiyo kwa wiki moja, chini ya Kampuni ya Airline AB Aviation ya Comoro, tangu ilipoingia mkataba wa kuikodi kutoka Fly Zanzibar.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted