Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich adaiwa kuwekewa sumu katika mazungumzo ya amani

Bilionea huyo alionyesha dalili zikiwemo macho mekundu na kuchubuka ngozi baada ya mazungumzo ya amani mjini Kyiv.

0
Roman Abramovich, Mmiliki wa Chelsea

Roman Abramovich adaiwa kuwekewa sumu mapema mwezi huu,mmiliki huyo wa klabu ya Chelsea mwenye umri wa miaka 55, ambaye anaiuza Chelsea akiwa chini ya vikwazo vya serikali, alionyesha dalili zikiwemo macho mekundu na kuchubuka ngozi baada ya mazungumzo ya amani mjini Kyiv.

Bilionea huyo na angalau wapatanishi wawili wa Kiukreni walionyesha dalili za kutiliwa sumu, ripoti tofauti kutoka Belingcat ikisema kwamba tukio hilo lilitokea usiku wa Machi 3. Wale walioathiriwa walichunguzwa asubuhi iliyofuata baada ya kusafiri magharibi hadi Lviv na kisha hadi katika mpaka wa Poland, ripoti ya Bellingcat imeongezwa.

Tangu wakati huo, Abramovich amepigwa picha katika uwanja wa ndege nchini Israel mnamo Machi 15 akionekana kuwa buheri wa afya.

Jaribio hilo la kutiliwa sumu linaripotiwa kutekelezwa na watu wenye msimamo mkali huko Moscow ambao walitaka kuhujumu mazungumzo ya kumaliza vita.

Inasemekana kuwa Abramovich alikuwa na dalili kama vile, ‘macho mekundu,kutiririkwa machozi ya mara kwa mara na yenye uchungu, na kuchubuka ngozi kwenye nyuso na mikononi.”

Mmiliki huyo wa Chelsea inasemekana alikuwa akisafiri kati ya Moscow, Ukraine na Uturuki tangu alipoamua kuiuza Chelsea Machi 2.

Kwa nini Abramovich anahusika katika mazungumzo ya amani?

Watu walio karibu na Abramovich wamedai kuwa amekuwa akihusika katika mazungumzo ya amani tangu vita vilipozuka mwishoni mwa mwezi Februari.

Ameonekana karibu na mpaka kati ya Belarus na Ukraine, na ndege zake za kibinafsi.

Baada ya kuwekewa vikwazo na serikali ya Uingereza mnamo Machi 10, mmiliki wa huyo wa Blues alielezwa kama “Bilionea mwenye uhusiano wa karibu” na Vladimir Putin kwa miongo kadhaa na amepata “manufaa ya kifedha” na “amekuwa akipata upendeleo” kutokana na uhusiano wake na Putin.

Umoja wa Ulaya (EU) kisha ukafuata mkondo huo na kumuwekea vikwazo Abramovich jambo ambalo lilisababisha matatizo kwa uendeshaji wa klabu ya Chelsea.

Walakini, katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na mazungumzo kwamba Chelsea wanataka kuongeza bei ya kilabu hadi viwango vya juu kabisa kwa klabu yoyote ile.

Wakiwa na matarajio kwamba mapato ya mauzo yanaweza hatimaye kwenda kwa Abramovich baada ya vikwazo alivyowekewa hatimaye kuondolewa.

Rekodi ya sasa ya mauzo ya juu zaidi ya klabu ni pauni bilioni 2.5, ambayo Joseph Tsai alinunua klabu ya NBA ya Nets.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted