Wahamiaji haramu 77 wakamatwa

Kati ya wahamiaji hao, wiki iliyopita walikamatwa 24 na wameshaondoshwa, leo wamekamatwa 24 mjini Geita, Chato wamekamatwa 15 na Bukombe wahamiaji 14 na wapo katika utaratibu wa kuwaondosha.

0

Wahamiaji haramu 77 kutoka Burundi, wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Geita, baada ya kuingia na kufanya shughuli  kinyume cha sheria.

Akizungumuza baada kuwashikilia baadhi ya wahamiaji hao, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Geita, Emmanuel Lukumai, amesema baadhi yao wamekutwa wakiendesha usafiri wa baiskeli za kibiashara maarufu kama daladala.

Amefafanua kati ya wahamiaji hao, wiki iliyopita walikamatwa 24 na wameshaondoshwa, leo wamekamatwa 24 mjini Geita, Chato wamekamatwa 15 na Bukombe wahamiaji 14 na wapo katika utaratibu wa kuwaondosha.

Kamanda Lukumai ameweka wazi, hayo ni matokeo ya operesheni ya siku 10 ya kuwasaka wahamiaji haramu, ambayo ilianza Alhamisi wiki iliyopita kuwasaka wanaoishi nchini kinyume na taratibu.

“Hawa (24) ni baadhi ya watu tuliowakamata, ambao ni raia wa Burundi, wanajishughulisha sana na uendeshaji wa daladala, ndiyo kazi zao wanaendesha, wengine wapo kwenye mashamba.

“Wengine tutafikiria namna ya kuwafikisha mahakamani, wengine tutawatoza faini maalumu, ili waweze kubadilisha mwenendo wao, wengine hawa wanajishughulisha, lakini hawana pasipoti ya nchi,” amesisitiza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted