Amuua mumewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kichogoni.

Chanzo cha tukio kimetajwa kuwa ni ugomvi uliotokana na mwanamke ambaye ni mtuhumiwa kuchelewa kurudi nyumbani na alipoulizwa ndipo ulizuka ugomvi uliopelekea kifo cha mwanaume.

0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya SACP, Ulrich Matei

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mwanamke Riziki  Henry (22), Mkazi wa Nditu Wilaya ya Rungwe mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya mume wake aitwaye Ayubu Aron (330,Mkazi wa Nditu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya SACP, Ulrich Matei amesema tukio hilo limetokea April 2,2022 majira ya saa 05:00 alfajiri huko Nditu Kata ya Suma, wilaya ya Rungwe ambapo mwanamke huyo anadaiwa kumpiga mumewe  na kitu butu kichwani na kumchoma na kitu chenye ncha kali kichogoni.

Baada ya tukio hilo, mhanga alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana kwa matibabu lakini mnamo tarehe 02.04.2022 majira ya saa 17:30 jioni alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo.

Chanzo cha tukio kimetajwa kuwa ni ugomvi uliotokana na mwanamke ambaye ni mtuhumiwa kuchelewa kurudi nyumbani na alipoulizwa ndipo ulizuka ugomvi uliopelekea kifo cha mwanaume.

 Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana kwa uchunguzi wa kitabibu, huku upelelezi ukiendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted