Wapeleka risasi kwa mganga wa kienyeji kwa ajili ya kufanyia zindiko

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu wawili raia wa Burundi wakiwa na risasi mbili za bunduki aina ya AK 47 ambazo walikuwa wakizipeleka kwa mganga kwa ajili...

0

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu wawili raia wa Burundi wakiwa na risasi mbili za bunduki aina ya AK 47 ambazo walikuwa wakizipeleka kwa mganga kwa ajili ya kuzifanyia zindiko ili wafaulu kwenye shughuli zao za ujambazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema watu hao walikamatwa wiki iliyopita kwenye Kijiji cha Lugenge wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Bavumilagie Salvatory (48) ambaye ni mganga wa kienyeji raia wa Burundi na Ndimgwaho Paskazia (48) Mkulima mkazi wa Kijiji cha Kumka nchini Burundi.

Kamanda Manyama alisema polisi wakiwa kwenye doria walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa watu hao na nyendo zao ndipo walipowawekea mtego na kuwakamata.

Katika hatua nyingine, watoto sita kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya Kigoma wenye umri wa kati ya miaka miwili hadi miaka sita wamekufa baada ya kutumbukia kwenye visima na madimbwi ya maji.

Kwa mujibu wa Kamanda Manyama watoto hao wamefariki baada ya kutumbukia kwenye visima vya maji na madimbwi huku sababu kubwa ikiwa ni wazazi kushindwa kusimamia ulinzi na usalama wa watoto hao wanapokuwa wanacheza.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Kamanda Manyama alisema watoto wawili ni kutoka Wilaya ya Kasulu, watoto wawili Wilaya ya Buhigwe, watoto wawili Wilaya ya Uvinza na watoto wawili katika Wilaya ya Buhigwe na kwamba vifo hivyo vilitokea kwenye kipindi cha Machi mwaka huu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted