Mamilioni ya Wasomali wapo katika hatari ya njaa: Mashirika ya Umoja wa Mataifa

Wasomali milioni sita au asilimia 40 ya watu sasa wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, kulingana na ripoti mpya ya Integrated Food Security Phase Classification

0

Mamilioni ya watu nchini Somalia wako katika hatari ya kukumbwa na njaa, huku watoto wadogo wakiwa katika hatari zaidi ya ukame unaozidi kuwa mbaya katika taifa hilo la Pembe ya Afrika, mashirika ya Umoja wa Mataifa yalionya Jumanne.

“Somalia inakabiliwa na hali ya njaa kutokana na kukosekana kwa mvua kwa kipindi kirefu na kupanda kwa bei ya vyakula na uhaba mkubwa wa fedha unaacha karibu asilimia 40 ya Wasomali hatarini,”mashirika yalisema katika taarifa.

Maeneo mengi ya Somalia yamekumbwa na ukame ambao pia umekumba mataifa mengine katika kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Ethiopia na Kenya, lakini mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuhusu upungufu mkubwa wa fedha ili kukabiliana na mzozo huo na kuepusha kujirudia kwa njaa ya mwaka 2011.

Wasomali milioni sita au asilimia 40 ya watu sasa wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, kulingana na ripoti mpya ya Integrated Food Security Phase Classification,hiyo ikiwa ni karibu ongezeko la mara mbili tangu mwanzoni mwa mwaka, mashirika hayo yalisema.

Taarifa ya pamoja ya WFP, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), wakala wa kibinadamu OCHA na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto lilisema maeneo yanayo kabiliwa na uhaba wa njaa yapo katika maeneo sita ya Somalia.

Walisema watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ndio walio katika mazingira magumu zaidi, huku upatikanaji wa chakula na maziwa ukiwa ni mdogo kwa sababu ya kupanda kwa bei ya bidhaa na masuala ya mifugo.

Takriban watoto milioni 1.4 wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri mwaka mzima, huku karibu robo moja wakikabiliwa na utapiamlo mkali, ilisema taarifa hiyo.

Kwa pamoja, mashirika ya kibinadamu yameweza kusambaza misaada kwa karibu watu milioni mbili lakini Umoja wa Mataifa ulionya kuhusu ‘pengo kubwa’ katika ufadhili na mpango wa 2022 unaotafuta dola bilioni 1.5 kufikia asilimia 4.4 tu ya lengo.

Katika njaa ya 2011, watu 260,000 — nusu yao wakiwa watoto chini ya umri wa miaka sita — walikufa kwa njaa au magonjwa yanayohusiana na njaa.

Maafa kutokana na matatizo mengine — sio migogoro — katika miaka ya hivi karibuni yamekuwa sababu kuu za watu kuhama makazi yao nchini Somalia, taifa lililokumbwa na vita ambalo liko miongoni mwa mataifa yaliyo hatarini zaidi na mabadiliko ya tabia nchi

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted