DR Congo: Wanajeshi ‘walevi’ waua watu 15

Wanajeshi wawili wamewaua kwa risasi jumla ya watu 15, ikilaumu shambulizi hilo kutokana na wanajeshi hao kulewa chakari.

0

Wanajeshi wawili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamewaua kwa risasi jumla ya watu 15 katika mashambulizi tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mamlaka ilisema Jumatatu, ikilaumu shambulizi hilo kutokana na wanajeshi hao kulewa chakari.

Mwanajeshi mmoja aliyelewa aliwaua abiria wanane na kuwajeruhi saba siku ya Jumatatu ndani ya boti kwenye Ziwa Tanganyika, msimamizi wa eneo la Fizi katika jimbo la Kivu Kusini Aime Kawaya Mutipula aliiambia AFP.

“Miongoni mwa waathiriwa, ni wanaume, wanawake na watoto,’ alisema.

“Amefungiwa,” aliongeza mratibu wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo Andre Byadunia, akizitaka “mamlaka kumfikisha mahakamani na kumhukumu.”

Siku ya Jumapili, askari mwingine alimpiga risasi na kumuua mlinzi wa kanali kabla ya kumuua kanali na raia watano huko Bambu, katika eneo la Djugu, mamlaka ya eneo hilo ilitangaza katika mkoa wa Ituri.

Kijiji “kiliamka Jumapili asubuhi kwa milio ya  risasi,” alisema afisa wa eneo hilo Claude Mateso.

Lakini, alieleza, ni askari mmoja ambaye alinyang’anywa silaha na wenzake jioni iliyotangulia kwa sababu alikuwa amelewa.

Muuaji, ambaye alikuwa amepata bunduki yake, hatimaye alipigwa risasi na askari mwingine ambaye alikimbia.

“Kilikuwa kisa cha kipekee na tunalaani vikali,” Luteni Jules Ngongo, msemaji wa jeshi la Ituri alisema.

“Tunasubiri kuelewa sababu halisi za kitendo hiki cha kutowajibika na uhalifu,” aliongeza.

Wakati huo huo katika eneo jirani la Kivu Kaskazini, watu sita walijeruhiwa na guruneti lililorushwa kwenye umati wa watu na askari waliokuwa wakijaribu kumkamata kijana katika kijiji cha Kisovu, eneo la Masisi, alisema katibu tawala wa eneo hilo Ngendahimana Eugee Gishoma.

Mikoa yote mitatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekumbwa na ghasia zinazohusishwa na makundi mengi ya watu wenye silaha kwa muda wa miaka 25 iliyopita.

Serikali imeweka Ituri na Kivu Kaskazini chini ya “hali ya kuzingirwa” tangu Mei mwaka jana, lakini vikosi vya usalama vimeshindwa kurejesha amani.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted