Bolt huenda ikasitisha huduma zake Tanzania

Kampuni hiyo huenda ikasitisha huduma zake kutokana na agizo la hivi karibuni la kutozwa ada ya huduma ya 15%.

0

Ripoti kutoka Tanzania zinafichua kuwa kampuni maarufu ya teksi, Bolt, huenda ikasitisha huduma zake nchini humo.

Kampuni hiyo huenda ikasitisha huduma zake kutokana na agizo la hivi karibuni la kutozwa ada ya huduma ya 15%.

Kampuni mbili kuu za usafiri nchini ni Bolt na Uber na ada hii inaathiri biashara zao.

Kulingana na Bolt, tayari inafanya mawasiliano na wadau husika.

Meneja wa Bolt kanda ya Afrika Mashariki, Kenneth Micah alisema

“Bolt imeomba kukutana na washikadau husika ili kujadili zaidi suala hili kwa matumaini ya kufikia kanuni bora za ushuru na kanuni za tume, hata tunapoendelea kutafuta njia mbadala za ushawishi zinazotolewa ndani ya mfumo wa kisheria ikiwa ni pamoja na mfumo wa udhibiti wa Latra,”

Latra ni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu ambayo inadhibiti huduma za teksi nchini Tanzania.

Mamlaka hiyo ndiyo yenye jukumu la kupanga nauli na mapitio ya nauli zilizopo.

Kulingana na Bolt, italazimika kusitisha biashara yake ikiwa hali itaendelea kuwa ilivyo kwa sasa.

Bolt ikisitisha huduma zake, basi soko litakuwa na kampuni ndogo kama Little na Ping.

Kwa sasa, Little hutoza 15% huku Bolt na Uber zinatoza 20% na 25% mtawalia.

Ingawa Bolt bado inajaribu kufanya uamuzi, Uber tayari ilisitisha operesheni yake nchini wiki jana.

Taarifa iliyotolewa na Uber Tanzania imeeleza kuwa kanuni za sasa za usimamizi wa sekta hiyo si rafiki nchini Tanzania na zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara ya usafiri, hivyo wanasitisha hadi hapo muafaka utakapopatikana.

Aidha Uber Tanzania imesema pamoja na wakati mgumu walionao hivi sasa, wako tayari kwa mazungumzo na mamlaka husika ili kujenga mazingira wezeshi ya kibiashara

Kampuni ya Bolt kwa upande wake inadai kwamba itaanza kufanya kazi tena ikiwa kutakuwa na mabadiliko mazuri.

Kulingana na Bolt, zaidi ya madereva 10,000 watalazimika kutafuta kazi kwingine ikiwa itasistisha huduma zake.

Bolt inafanya kazi katika masoko saba barani Afrika ikiwa ni pamoja na Nigeria, Kenya, Afrika Kusini, Uganda, na Ghana.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted