NCCR Mageuzi yaweka mgomo kushiriki vikao vya kikosi kazi

Chama hicho cha siasa za upinzania nchini Tanzania kimesema kushiriki mkutano huo ni kupoteza muda  na kutumia vibaya rasilimali za Watanzania badala ya kujadili masuala muhimu ya uchumi...

0

Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema hakitashiriki katika utoaji wa maoni na mapendekezo kwa kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia, kikisema kufanya hivyo ni kupoteza muda.

Chama hicho cha siasa za upinzania nchini Tanzania kimesema kushiriki mkutano huo ni kupoteza muda  na kutumia vibaya rasilimali za Watanzania badala ya kujadili masuala muhimu ya uchumi kwa ajili ya wananchi

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Ilala jijini hapa, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye amesisitiza kushikilia msimamo wao wa awali wa kutoshirikia mchakato huo kwasababu hawajui muundo wake upoje, hatukushiriki kwenye uundwaji wake na kitu gani wanafanya.

 ‘’Huku ni kupoteza muda na rasilimali za watanzania wakati kuna mambo mengi ya kufanya katika taifa letu ili kukuza uchumi,” amesema Simbeye

NCCR Mageuzi inaungana na Chadema ambayo tangu awali ilikataa kushiriki mkutano wa vyama vya siasa ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania na kufanyika jijini Dodoma Desemba 2021.

Mkutano huo ndiyo ulioansisha kikosi kazi hicho kinachoratibu maoni ya wadau.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, leo Mei 5 ilikuwa ni zamu ya vyama vya siasa kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu maeneo tisa yaliyochambuliwa na kupendekezwa na kikosi kazi hicho.

Hata hivyo Katibu wa kikosi kazi hicho, Sisty Nyahoza amesema mchakato huo utaanza rasmi Mei 9 kutokana na kuingiliana na ratiba za sikukuu.

Ameongeza kuwa kwenye mwaliko huo kuna ajenda ya katiba mpya ambayo kwa mapendekezo ya kikosi hicho walitaka iwe baada ya mwaka 2025.

“Katiba mpya ni sasa sio mwaka 2025 pia wanasema tukajadili mikutano ya hadhara na ndani ya chama wakati vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria yani leo sisi tukajadili uhuru wetu ambao tayari tumepewa,” amesema Simbeye

Mbali na hoja hiyo, Simbeye amegeukia pngezeko la bei ya mafuta akihoji sababu ya bei ya Bara kutofautiana na ya Zanzibar.

“Zanzibar na huku Bara bei ni tofauti haya ndio mambo ya kujadiliana sio kupoteza muda na kikosi kazi ambacho hakina maslahi yoyote kwa nchi,” amesema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted