Bobi Wine ndani ya Baraza Kuu la Chadema

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amethibitisha ujio wa Bob Wine leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kikao hicho, kitakachotanguliwa...

0

Aliyekuwa mgombea wa urais wa Uganda kwa tiketi ya chama cha National Unity (NUP),Platform Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, anatarajiwa kuwa mgeni maalumu katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema litakalofanyika Jumatano Mei 11 katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amethibitisha ujio wa Bob Wine leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kikao hicho, kitakachotanguliwa na kikao cha kamati kuu itakayoketi kesho Jumanne Mei 10, 2022.

“Bob Wine ambaye ni kiongozi chama kikuu cha upinzani cha NUP cha Uganda atakuwa mgeni wetu mwalikwa maalum katika kikao cha baraza kuu litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City,” amesema Mrema.

Chadema kitafanya kikao cha baraza kuu litakalokuwa na ajenda tano na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho, watakaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mrema, Baraza Kuu litakuwa na ajenda tano ambayo ni mpango mkakati wa chama kwa miaka tano pamoja na mpango kazi wa mwaka.

“Katika mpango kazi wa miaka mitano, maana yake tunakwenda kukubaliana namna ya kuvuka kuanzia sasa hadi baada uchaguzi mkuu wa 2025, tunakwenda katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kwenye mpango mkakati huu tutajadili kwa kina masuala ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

“Baada ya baraza kuu tutawaeleza kile ambacho tumekubaliana katika Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Ajenda nyingine itakuwa ni uchaguzi ndani ya chama ambao ratiba yake imekaribia na baraza kuu lina mamlaka kutangaza tarehe rasmi ya kuanza mchakato huu unaonzia ngazi ya chini,” amesema Mrema.

Mrema amesema ajenda nyingine itakuwa ni rufaa ya nidhamu iliyokatwa na wabunge 19 wa viti maalumu wakiongozwa na Halima Mdee wakipinga kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho iliyoketi mwisho mwa mwaka 2020.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted