Amerika: Watoto 19 na walimu wawili wauawa kwenye shambulio

Mshambuliaji Salvador Ramos aliua watu 21 katika darasa moja

0
UVALDE, TX – MAY 25: Askari wa Jimbo la Texas akipokea maua kwa ajili ya waathirwa wa shambulio la risasi lililofanyika jana katika Shule ya Msingi ya Robb ambapo watu 21 waliuawa, wakiwemo watoto 19, Mei 25, 2022 huko Uvalde, Texas.Mshambuliaji aliyetambulika kama Salvador Ramos mwenye umri wa miaka 18, aliripotiwa kuuawa na maafisa wa polisi, Jordan Vonderhaar/Getty Images/AFP (Photo by Jordan Vonderhaar / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP)

Jumuiya ya watu wa Latino katika jimbo la Texas walijawa na huzuni Jumatano baada ya kijana kuenda hadi katika shule ya msingi na kuwaua watoto wadogo 19 na walimu wawili, katika msururu wa hivi punde wa mashambulizi mabaya ya risasi nchini Amerika.

Maelezo ya ukatili huo, waathiriwa na mshukiwa mwenye umri wa miaka 18 — ambaye aliuawa na polisi — yaliibuka wakati Amerika ikikabiliana na ufyatuaji risasi mbaya zaidi shuleni tangu mkasa wa Sandy Hook huko Connecticut muongo mmoja uliopita.

“Watu katika mji huu wamevunjika moyo,” alisema Adolfo Hernandez, ambaye mpwa wake alikuwa akisomea shule ya msingi ya Robb Elementary huko Uvalde, jumuiya ndogo iliyo umbali wa takriban saa moja kutoka mpaka wa Mexico.

“Tunahisi kama kuna wingu jeusi juu ya mji huu,” aliiambia AFP.

“Unataka tu kujibana na kuamka kutoka kwa ndoto hiyo mbaya.”

Akiwa amejawa na huzuni na hasira, Rais Joe Biden alihutubia taifa saa chache baada ya shambulio hilo, na kutoa wito kwa wabunge kutunga sheria kali zaidi kukomesha mashambulizi ya bunduki.

Biden aliuliza, sauti yake ikiwa imejaa huzuni.

Huko Uvalde, polisi walikuwa wameweka vizuizi katika eneo karibu na shule na kulikuwa na msongamano mdogo wa wapiti njia.

Mshambuliaji huyo aliyetambuliwa kama Salvador Ramos, alikuwa mkazi wa mji huo na raia wa Marekani.

Kwa mujibu wa maafisa wa Idara ya Usalama wa Umma wa Texas, Ramos alimpiga risasi nyanyake kabla ya kuelekea Shule ya Msingi ya Robb mwendo wa saa sita mchana.

Mshukiwa alidhulumiwa

Maelezo yameibuka kuhusu mshukiwa kama kijana aliyejawa na matatizo — alidhulumiwa mara kwa mara kutokana na tatizo la kuongea lililojumuisha kigugumizi na inadaiwa kuwa alijikata uso “kwa ajili ya kujifurahisha,” rafiki yake wa zamani wa Ramos, Santos Valdez, aliiambia The Washington Post.

Valdez alisema alikuwa rafiki ya Ramos lakini sio tangu hali ya Ramos alipoanza kuzorota.

Ramos aliua watu wote 21 katika darasa moja, CNN na vyombo vingine vya habari viliripoti.

Familia za mji huo wa Uvalde zilipokuwa zikisambaza habari hizo kwenye mitandao ya kijamii, majina ya watoto waliouawa, wengi wao wakiwa wa urithi wa Latino, yalianza kutolewa: Ellie Garcia, Jayce Carmelo Luevanos, Uziyah Garcia..

Zaidi ya watoto kumi na wawili pia walijeruhiwa katika shambulio katika shule hiyo, shule inayokuwa na zaidi ya wanafunzi 500 wenye umri wa kati ya miaka saba hadi 10, wengi wao wakiwa ni Wahispania na wasiojiweza kiuchumi

Mshambuliaji huyo aliuawa na maafisa wa polisi.

Mwalimu wa darasa la nne Eva Mireles alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa akijaribu kuwalinda wanafunzi wake, shangazi yake Lydia Martinez Delgado aliambia New York Times.

Alisema Mireles alijivunia kufundisha watoto wa urithi wa Latino.

Kumekuwa na ufyatuaji risasi uliosababisha vifo vya watu wengi — ambapo watu wanne au zaidi walijeruhiwa au kuuawa — mnamo 2022 mwaka huu, kulingana na Kumbukumbu ya Ghasia ya Bunduki iliyorekodi matukio 213 kama haya.

Ufyatulianaji wa risasi wa Uvalde ulikuwa tukio baya zaidi tangu shambulio la Sandy Hook la 2012 huko Connecticut, ambapo watoto 20 wa shule ya msingi na wafanyikazi sita waliuawa.

Seneta Chris Murphy, mwanademokrasia kutoka Connecticut, ambapo shambulizi la risasi ya Sandy Hook ilifanyika,

“Hili si tukio la kawaida, watoto hawa hawakubahatika. Hii inatokea tu katika nchi hii na si mahali pengine popote,” Murphy alisema kwenye Seneti huko Washington.

Shambulio la mauaji huko Texas linafuatia mfululizo wa mauaji ya watu wengi nchini Marekani mwezi huu: hivi karibuni mnamo Mei 14 kijana mwenye umri wa miaka 18 aliyejitangaza kuwa wa itikadi kali ya watu weupe aliwapiga risasi watu 10 kwenye duka la mboga na kuwaua huko Buffalo, New York.

Licha ya ufyatuaji wa risasi wa mara kwa mara wa majeruhi wengi, mipango mingi ya kurekebisha kanuni za bunduki imeshindwa katika Bunge la Marekani, na kuacha majimbo na mabaraza ya mitaa kuimarisha – au kudhoofisha – vikwazo vyao wenyewe.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted