Nigeria imethibitisha visa 21 vya ugonjwa wa Monkeypox tangu Januari

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria (NCDC) kilisema kufikia Jumapili visa 66 vinavyoshukiwa kuwa vya Monkeypox vimeripotiwa katika majimbo tisa kati ya 36 nchini humo na katika mji...

0
Picha hii iliyotolewa na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa ilipigwa mwaka 1997 wakati wa uchunguzi wa mlipuko wa monkeypox, ambao ulitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), (Photo by Brian W.J. Mahy / Centers for Disease Control and Prevention

Nigeria imethibitisha visa 21 vya ugonjwa wa Monkeypox tangu mwanzoni mwa mwaka huu, shirika la kudhibiti magonjwa nchini humo lilisema.

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria (NCDC) kilisema kufikia Jumapili visa 66 vinavyoshukiwa kuwa vya Monkeypox vimeripotiwa katika majimbo tisa kati ya 36 nchini humo na katika mji mkuu Abuja.

Kati ya visa hivyo 21 vilithibitishwa baadaye kama Monkey Pox, kisa kimoja kikiwa cha mwanamume wa miaka 40 ambaye pia alikuwa na ugonjwa wa figo.

“Kati ya visa vilivyoripotiwa mnamo 2022 hadi sasa, hakujawa na ushahidi wowote wa maambukizi mapya au yasiyo ya kawaida ya virusi, wala mabadiliko katika udhihirisho wake wa kliniki,” NCDC ilisema.

Visa sita kati ya hivyo viligunduliwa mnamo Mei, ilisema.

NCDC ilisema uwezekano wa waNigeria kuambukizwa virusi vya monkeypox ni kubwa kulingana na tathmini ya hivi majuzi iliyofanywa, lakini athari za kiafya zilikuwa ndogo.

“Hali ya sasa nchini Nigeria na duniani kote haijaonyesha tishio kubwa kwa maisha au jamii ambayo inaweza kusababisha ugonjwa mbaya au kiwango cha juu cha vifo,” ilisema.

Shirika hilo limewataka wananchi kufahamu hatari hiyo na kumjulisha daktari iwapo watakuwa na dalili zozote za ugonjwa huo.

Monkeypox inafanana na ndui lakini haina atahri kubwa.

Dalili za awali ni pamoja na homa kali, nodi za lymph kuvimba na upele unaofanana na tetekuwanga.

Watu wengi hupona ndani ya wiki kadhaa.

Virusi vinaweza kupitishwa kwa wanadamu na wanyama walioambukizwa.

Maambukizi kutoka kwa mtu hadi kwa mtu ni nadra sana — wataalam wanasema maambukizi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine aliyeambukizwa na ambaye ana malengelenge kwenye ngozi.

Hakuna matibabu mahususi lakini chanjo dhidi ya ndui imepatikana kuwa na ufanisi wa takriban asilimia 85.

Monkeypox iligunduliwa kwa mara ya kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka wa 1970.

Kulipuka kwake katika nchi zisizo na ugonjwa kumewatia wasiwasi wataalam, ingawa visa vilivyoripotiwa hadi sasa vimekuwa vyepesi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted