Sabaya amwaga chozi Mahakamani, asema hana imani na Mwendesha mashtaka

Kwa upande wake Sabaya aliyeomba kuongea licha ya Hakimu kueleza kuwa maombi yake hayata zingatiwa kwa sasa alieleza mahakamani hapo kuwa hana imani na Mwendesha mashtaka wa serikali...

0

Aliye kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya leo Juni 1.2022 amefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Moshi Mkoani Kilimanjaro akiwa na wenzake 4 kwa makosa saba ya uhujumu uchumi.

Akisoma mashtaka yanayomkabili Sabaya na wenzake ,Mwendesha mashataka wa serikali Tumaini Kweka amesema kuwa Sabaya na wenzake wanne Sylvester Nyegu, John Odemba Aweyo,Nathan Msuya na Antheo Boniface Assey wanashtakiwa na makosa saba ya uhujumu uchumi ikiwemo kuongoza genge la uhalifu,kutenda kinyume na mamlaka yake,kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.

Hata hivyo Wakili upande wa utetezi Hellen Mahuna ameiomba Mahakama hiyo kufuata sheria ili kutenda haki akidai kuwa wateja wake na Mahakama ya Arusha haikupata kibali halali cha kuwatoa washtakiwa gereza la Kisongo Arusha na kuwapeleka gereza la Karanga Moshi.

“Mhe.Mahakama imefanya kinyume (irregular) kuwaleta washtakiwa Moshi bila wao kujua wala mawakili wao kupewa taarifa nimestukia kuona tuu wateja wangu wako Moshi wakati mimi naendelea na kesi nyingine” alieleza Wakili Mahuna.

Kwa upande wake Sabaya aliyeomba kuongea licha ya Hakimu kueleza kuwa maombi yake hayata zingatiwa kwa sasa alieleza mahakamani hapo kuwa hana imani na Mwendesha mashtaka wa serikali Tumaini Kweka.

“Mhe.Hakimu sina imani na Mwendesha mashtaka wa serikali Tumaini Kweka kwa kuwa anatokea Wilaya ya Hai Kijiji cha Makoa nilipo kuwa nafanyia kazi,anatumikaa kisiasa na anachuki, naomba Rais Samia alione hili linalofanyika Kilimanjaro katika kesi hii,hawa ninaoshtakiwa nao wanateseka bure pamoja na mimi ikiwa huyu Kweka ataendelea na kesi hii”Aliomba Sabaya huku akilia.

Kufuatia mabishano hayo Hakimu Mkazi Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza shauri hilo Salome Mshasha aliahirisha usikilizaji wake kwa muda wa dakika kumi (10) ili apate kupitia sheria juu ya yaliyotajwa huku akidai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayo mkabili Sabaya na wenzake.

Kufuatia hayo Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 2 ya mwaka 2022 inayomkabili Sabaya na wenzake 4 imeahirishwa mpaka Juni 7,Mwaka huu kwa ajili ya kuja kutajwa.

Itakumbukwa haya mashtaka mapya kwa Sabaya na wenzake wanne ambapo yamekuja wakati washtakiwa hao wakisubiri hukumu ya kesi ya awali ya Uhujumu Uchumi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha..

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted