Watoto 12,131,049 wapatiwa chanjo ya Polio nchini Tanzania.

Waziri wa Afya nchini humo ,Ummy Mwalimu amesema Mei 18 , 2022, Wizara ya Afya ilizindua awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya...

0

Watoto 12,131,049 sawa na asilimia 117.8 wamepatiwa chanjo ya matone dhidi  ya ugonjwa wa Polio kwa watoto chini ya miaka mitano kati ya watoto 10,295,316 waliolengwa nchini Tanzania.

Waziri wa Afya nchini humo ,Ummy Mwalimu amesema Mei 18 , 2022, Wizara ya Afya ilizindua awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio hapa nchini.

” Uzinduzi wa kampeni hii ya kitaifa ilifanyika katika viwanja vya Chinangali Park, vilivyoko katika Jiji la Dodoma na utekelezaji wake kuendelea kwa siku nne mfululizo kuanzia Mei  18 hadi 21 Mei, 2022 ikihusisha mikoa yote  hapa nchini.”

Ummy amesema  Kampeni hiyo ililenga kuwapatia chanjo watoto 10,295,316 kwa Tanzania bara.

Amesema Ufanisi wa utoaji wa chanjo hiyo umetofautiana kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine kwa asilimia.

“kwa ngazi ya mikoa, Mkoa wa Ruvuma ulivuka lengo kwa asilimia 131, ikifuatia na Shinyanga  asilimia 128, Rukwa asilimia 123, Pwani asilimia  122,  Arusha  asilimia 122, Mbeya, Geita, Dar es Salaam na Simiyu yote ina asilimia 121.

Kwa upande wa  Singida, Dodoma na Tabora asilimia  118 , Kigoma, Njombe, Katavi asilimia 117, Morogoro asilimia 116, Mara, Mtwara, Lindi na Tanga  asilimia 115, Kilimanjaro na Mwanza asilimia 114, Manyara na Iringa asilimia  113, Songwe na Kagera asilimia111.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted