Serikali ya Tanzania kutumia trilioni 9 kulipa deni

Wizara ya Fedha na Mipango nchini Tanzania imeliomba Bunge kuidhinisha shilingi trilioni 14.94 ikiwa ni  bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 huku shilingi trilioni 9.09 zikienda katika kulipa...

0

Wizara ya Fedha na Mipango nchini Tanzania imeliomba Bunge kuidhinisha shilingi trilioni 14.94 ikiwa ni  bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 huku shilingi trilioni 9.09 zikienda katika kulipa deni la Serikali.

Waziri wa Fedha na Mipango nchini humo, Dk Mwigulu Nchemba amesema kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 13.62 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.32 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Aidha, Dk Mwigulu amesema katika mwaka 2022/23, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini (TADB) imepanga kutoa mikopo ya shilingi bilioni 78 kwa sekta ya viwanda, hususani viwanda vya mafuta ya kula na sukari katika Mkoa wa Kigoma, Shinyanga na Manyara.

Kwa mujibu wa Dk. Mwigulu ni kwamba Mikopo hiyo inatarajia kupunguza upungufu wa mafuta ya kula na sukari nchini Tanzania. 

Aidha, amesema benki imepanga kutoa mkopo wa takribani shilingi bilioni 130 kwa ajili ya ununuzi wa pamba na kahawa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted