Miaka 25 jela kwa kukutwa na ngozi mbili za chui

Awali mtuhumiwa aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwasababu ni kosa lake la kwanza na amefanyiwa upasuaji hivyo hawezi kufanya kazi ngumu na ana familia kubwa yenye watoto sita na...

0

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu Ezel Kasenegala (35), kifungo cha miaka 25 au faini ya shilingi milioni 163.670 baada ya kumtia hatiani kwa kukutwa na ngozi mbili za chui zilizokuwa na thamani ya shilingi milioni 16.367.

Kasenegala ambaye ni mkulima na mkazi wa Lulanzi wilayani Kilolo alikamatwa akiwa anauza ngozi hizo kwa shilingi 500,000 kwa kila moja.

Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa, amesema mtuhumiwa alikamatwa Mei 12, 2020 katika  eneo la ipogolo na amekutwa na hatia ya kukutwa na ngozi mbili za chui “Wasamaria wema walilitaarifu Jeshi la Polisi ndipo wakaweka mtego wa kumkamata wakijifanya ni wanunuzi wa ngozi hizo za chui”

Mwendesha mashtaka wa Serikali Alex Mwita, ameiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na jamii yenye matendo kama hayo.

Awali mtuhumiwa aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwasababu ni kosa lake la kwanza na amefanyiwa upasuaji hivyo hawezi kufanya kazi ngumu na ana familia kubwa yenye watoto sita na wote wanamtegemea lakini hata hivyo Mahakama imemuhukumu kifungo cha miaka 25 au faini ya shilingi million 163.670.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted