Upinzani wa Afrika Kusini waitaka FBI kuchunguza kashfa ya wizi katika shamba la Ramaphosa

Ramaphosa anashutumiwa kwa kuficha polisi na mamlaka ya ushuru wizi wa pesa kutoka kwa nyumba yake ya kifahari ya shambani katika mkoa wa kaskazini wa Limpopo.

0
Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini

Chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini Afrika Kusini Jumanne kilisema kinatafuta usaidizi wa Ofisi ya FBI ya Marekani kuchunguza wizi wa fedha wa Rais Cyril Ramaphosa wa mwaka 2020.

Ramaphosa anashutumiwa kwa kuficha polisi na mamlaka ya ushuru wizi wa pesa kutoka kwa nyumba yake ya kifahari ya shambani katika mkoa wa kaskazini wa Limpopo.

Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance (DA) John Steenhuisen aliambia kikao cha wanahabari kwamba chama chake kiliiandikia FBI Pretoria Field Office “kuomba wachunguze madai ya uwezekano wa ufujaji wa pesa na rais.”

Mapema mwezi huu, mkuu wa zamani wa jasusi wa Afrika Kusini Arthur Fraser aliwasilisha malalamiko polisi akidai wezi waliiba pesa taslimu dola milioni 4 kutoka kwa shamba la Ramaphosa, ambapo pesa hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya samani.

Fedha hizo zilitokana na mauzo ya wanyama katika shamba la Ramaphosa la Phala Phala anapofuga ngombe na wanyama pori huko Bela Bela.

Fraser alimshutumu mkuu wa nchi kwa kuandaa utekaji nyara na kuwahoji majambazi, na kisha kuwapa hongo ili wanyamaze.

Ramaphosa amekiri wizi huo lakini anakanusha madai ya utekaji nyara na hongo, akisema aliripoti wizi huo kwa polisi.

Lakini DA ilisema inaiomba FBI kufikiria kuchunguza chanzo cha fedha hizo, jinsi pesa hizo zilivyoletwa nchini na kama zilitangazwa kwa mamlaka kabla ya kupelekwa kwa shamba la Ramaphosa.

“Muamala wa fedha ndani ya Afrika Kusini unaohusisha dola milioni 4 unatiliwa shaka sana, na zaidi kwa vile fedha hizo zilifichwa kwenye samani, na wizi wake ulichunguzwa bila rekodi na kufichwa,” alisema Steenhuisen.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted