Polisi Dar yawashikilia watu 23 kwa tuhuma za utapeli na kufanya biashara ya ngono

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema waliokamatwa ni  watuhumiwa waliokuwa wakijifanya wakuu wa shule, waganga wa kienyeji, ndugu wa waathirika, wahudumu wa makampuni...

0
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 23 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya utapeli kwa njia ya mtandao.

Kukamatwa kwa watu hao ni matokeo ya oparesheni maalum iliyofanywa na kanda hiyo kwa kushirikiana na timu maalumu ya Kuzuia na Kupambana na Uhalifu wa Mtandaoni.

Operesheni hiyo iliyofanyika kati ya Mei 18 hadi Juni 26 ilifanyika pia katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro ambapo watuhumiwa wengine walikamatwa huko.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema waliokamatwa ni  watuhumiwa waliokuwa wakijifanya wakuu wa shule, waganga wa kienyeji, ndugu wa waathirika, wahudumu wa makampuni ya simu au mawakala wa Freemason.

Amesema watuhumiwa hao huwatumia watu ujumbe mbalimbali kupitia namba tofauti za simu na kujifanya wanania ya kusaidia watu badala yake huishia kuwaibia.

Miongoni mwa waliokamatwa ni Julius Simon Mwabula (20) ambaye ni mkazi wa Ifakara Morogoro sambamba na wenzake 22.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo ikiwemo hivyo ni kama Kompyuta mpakato 2, kompyuta ya mezani 1, simu za aina tofauti 28, flash 2, modem ya mitandao yote na kadi za simu za mitandao mbalimbali zaidi ya 50.

Katika operesheni hiyo wamekamatwa pia wanawake wawili kwa kosa la kufanya biashara ya ngono mtandaoni na kusambaza picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted