Mwanawe dikteta, Ferdinand Marcos Jr. ala kiapo cha kuwa Rais wa Ufilipino

Amenufaika kutokana na taarifa potofu kwenye mitandao ya kijamii zinazowalenga wapiga kura wengi vijana ambao hawana kumbukumbu ya ufisadi, mauaji na dhuluma nyinginezo zilizofanywa wakati wa utawala wa...

0

Rais Mpya wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr akila kiapo kama rais wa Ufilipino huku mkewe Louise akitazama, wakati wa sherehe katika Jumba la Makumbusho la Kitaifa huko Manila mnamo Juni 30, 2022.(Photo by Ted ALJIBE / AFP)

Ferdinand Marcos Jr, anayejulikana kwa jina la utani ‘Bongbong’ alimrithi Rodrigo Duterte katika wadhifa wa juu siku ya Alhamisi baada ya ushindi wake wa kishindo katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Ushindi wake ulifuatia siku nyingi za kusafisha jina la familia yake na kuimarisha ushirikiano na familia pinzani zinazodhibiti maeneo makubwa ya nchi.

Katika kipindi cha miaka 36 tangu ghasia za watu kumkpindua babake na kuifukuza familia hiyo hadi uhamishoni Marekani, akina Marcos wamekuwa wakijenga upya wasifu wao wa kisiasa.

Licha ya wasiwasi wa baba yake kumhusu kuwa ni mtu asiyejali na mvivu, Marcos Jr, 64, alifikia wadhifa wa juu kabisa nchini humo.

Baada ya kushindwa kwa kiasi kidogo katika kinyang’anyiro cha makamu wa rais na Leni Robredo katika uchaguzi wa 2016, aliazimia kuwa kinyang’anyiro cha urais mnamo Mei 9 kingekwenda tofauti.

Akiapa kuunganisha nchi, Marcos Jr alitoa ahadi nyingi ikiwemo  kuongeza nafasi za kazi na kukabiliana na kupanda kwa bei katika nchi hiyo ya kipato cha chini.

Marcos alisema mwezi uliopita ‘alinyenyekezwa’ na mafanikio yake kwenye uchaguzi huo na akaapa ‘daima kujitahidi kufikia ukamilifu’

“Nataka kufanya vyema, kwa sababu rais anapofanya vyema nchi inafanya vyema, na ninataka kufanya vyema kwa ajili ya nchi hii,’ aliwaambia waandishi wa habari baada ya Congress kuidhinisha rasmi matokeo ya uchaguzi.

Akikulia katika ikulu ya rais huko Manila, Marcos Jr alitaka kuwa mwanaanga kabla ya kufuata nyayo za babake katika siasa.

Alihudumu kama makamu wa gavana na mara mbili kama gavana wa ngome ya kaskazini ya familia ya jimbo la Ilocos Norte, na pia aliwahi kuhudumu katika Baraza la Wawakilishi na Seneti.

Mamake Imelda mwenye umri wa miaka 92, alisema alikuwa na ndoto ya yeye kuwa kiongozi wa nchi.

Uhusiano wa Marcos Jr na babake, ambaye utawala wake ulikuwa wa ukandamizaji na umwagaji damu, umemfanya kuwa mmoja wa wanasiasa wenye uhusiano na mwanasiasa mwenye msimamo mkali zaidi nchini humo.

Amenufaika kutokana na taarifa potofu kwenye mitandao ya kijamii zinazowalenga wapiga kura wengi vijana ambao hawana kumbukumbu ya ufisadi, mauaji na dhuluma nyinginezo zilizofanywa wakati wa utawala wa miaka 20 wa mzee Marcos.

Kampeni yake iliimarishwa na kuungana na Sara Duterte — ambaye alipata kura nyingi zaidi kumliko Marcos na kashinda wadhfa wa kuwa makamu wa rais kwa urahisi — pamoja na kuungwa mkono na viongozi wengine wa kisiasa.

Historia ya Marcos Jr na Duterte kama vizazi vya viongozi wa kimabavu imetia hofu makundi ya kutetea haki na makasisi wengi wanaohofia kuwa watatumia ushindi wao kujikita madarakani.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted