Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi ajiuzulu

Kujiuzulu kwa Draghi kumekuja baada ya vyama kadhaa muhimu katika muungano wake  vuguvugu lenye nguvu la 5-Star, chama kikubwa zaidi katika serikali ya mseto ya nchi hiyo, kususia...

0
Mario Draghi, Waziri Mkuu wa Italia (Photo by Andreas SOLARO / AFP)

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwake kwa Rais Sergio Mattarella siku ya Alhamisi, na kutumbukiza uchumi wa tatu kwa ukubwa wa Umoja wa Ulaya katika machafuko mapya ya kisiasa.

Kujiuzulu kwa Draghi kumekuja baada ya vyama kadhaa muhimu katika muungano wake  vuguvugu lenye nguvu la 5-Star, chama kikubwa zaidi katika serikali ya mseto ya nchi hiyo, kususia kura ya imani na serikali Jumatano usiku.

Mattarella, ambaye alikubali kujiuzulu, amepangwa kukutana na maspika wa Bunge Alhamisi mchana, ikulu ya rais ilisema katika taarifa.

Hatua inayofuata sasa ni kufanyika kwa uchaguzi wa haraka.

Wiki iliyopita, Draghi alitangaza kujiuzulu kwa mara ya kwanza baada ya vuguvugu la 5 Star kuondoa ungwaji mkono wake katika kura ya imani ya bunge kuhusu kifurushi maalum cha fedha kilichoundwa kukabiliana na mzozo wa gharama ya maisha ya Italia.

Draghi alikuwa amesema hapo awali kwamba hataongoza serikali ambayo haikujumuisha 5-Star.

Kujiuzulu huko, hata hivyo, kulikataliwa na Rais wa Italia Sergio Mattarella, ambaye alimtaka abaki na kutafuta suluhu.

Siku ya Alhamisi, FTSEMIB, soko kuu la hisa la Italia, lilikuwa lilushuka zaidi ya 2.5% baada ya serikali ya nchi hiyo kuachwa katika hatari ya kuporomoka.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted