Bwege kumpigia kampeni Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu Kenya

Uchaguzi wa Kenya unatarajiwa kufanyia Agosti 9 Mwaka huu,ambapo mpinzani mkubwa wa Raila Odinga  katika Uchaguzi huo ni Naibu Rais Dk William Ruto.

0

Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, kwa tiketi ya ACT- Wazalendo, Suleiman Bungara maarufu ‘Bwege’, anatarajiwa kumnadi mgombea urais wa Kenya kupitia muungano wa Azimio  la Umoja, Raila Odinga.

‘Bwege’  ndio mwanasiasa wa kwanza kutoka Tanzania kupewa heshima hiyo na Timu ya Kampeni ya Azimio la Umoja. 

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Uenezi, Janeth Rithe, imeeleza kuwa ‘Bwege’ ameshaondoka kuelekea nchini Kenya. 

Uchaguzi wa Kenya unatarajiwa kufanyia Agosti 9 Mwaka huu,ambapo mpinzani mkubwa wa Raila Odinga  katika Uchaguzi huo ni Naibu Rais Dk William Ruto.

Kura mbali mbali za maoni zilizofanyika nchini Kenya,zinaonyesha Raila Odinga,anayeungwa mkono na Rais Uhuru Kenyata,amemuacha kwa Mbali Ruto.

Kumbukumbu za mtandaoni zinaonesha kuwa hotuba za  ‘Bwege’ ndani na nje ya Bunge zinafuatiliwa na kupendwa nchini Kenya, hali iliyomfanya apate mialiko kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini humo, Kati ya mwaka 2020-2022.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted