Bilioni 17 zatolewa kuimarisha huduma ya mama na mtoto nchini Tanzania       

Benki ya Dunia imetoa msaada wa shilingi bilioni  17 kwa serikali ya Tanzania, kwa ajili ya kuimarisha huduma ya mama na mtoto.

0

Benki ya Dunia imetoa msaada wa shilingi bilioni  17 kwa serikali ya Tanzania, kwa ajili ya kuimarisha huduma ya mama na mtoto.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati alipokutana na wadau kutoka Shirika la Global Financing Facility (GFF), kutoka Benki ya Dunia ambao wanafadhili mradi wa Kitita cha Uzazi Salama katika hospitali ya Rufaa ya Bombo.

Amesema fedha hizo zinatarajiwa kutumika katika ununuzi wa vifaa, kuwajengea uwezo watumishi wa afya, ili kubaini changamoto za mama mjamzito katika hatua ya awali na hivyo kuweza kudhibiti madhara zaidi.

“Wadau wa GFF wamefadhili huduma ya mama na mtoto katika mikoa mitano hapa nchini na tayari matokea ya awali yameonesha kupungua Kwa vifo kwa zaidi ya asilimia 50,”amesema Ummy Mwalimu.

Naye Meneja Mradi wa Kitita cha Uzazi Salama Dk Pascal Mdoe, amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Manyara, Tabora, Shinyanga, Geita na Mwanza.

“Mradi umeweza kufika hospitali 30 katika Awamu ya Kwanza, lakini awamu ya pili tunatarajia kufikia hospitali 100, lengo ni kuhakikisha tunamalizia changamoto ya vifo vya uzazi na watoto wachanga,”amesema Dk Mdoe

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted