Uber/Bolt kurudisha tena huduma nchini Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo ametoa taarifa hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

0

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesema, kampuni za usafiri kwa njia ya mtandao Bolt na Uber zinatarajia kurejea kutoa huduma za usafiri nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo ametoa taarifa hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Suluo amesema wamesikia kilio cha kampuni hizo na wameitana kukaa meza moja kwa mazungumzo na tayari wamekubaliana kutatua tatizo ili kurejesha huduma.

“Uber walijitoa baada ya tangazo la Latra la nauli na tiketi za mtandao ambao uliwataka kutoza tozo haalali kwa amri ya kutekelezwa na wakafungua kesi Baraza la Ushindani kupinga maamuzi yetu.”

“..Bolt waliendelea kutoa huduma lakini baadae nao wakaleta taarifa kuwa wanaenda kusitisha huduma lakini tuliwaita tukiamini katika mazungumzo” amesema Suluo

Latra wametoa taarifa hizo kipindi ambacho kampuni hizo kwa nyakati tofauti, walisitisha kutoa huduma za usafiri za magari na kubaki na bodaboda pamoja na bajaji.

“Tuliwaita wakaja na wawakilishi wao wa Afrika, tukaanza Septemba 5-8, 2022 tumemaliza mazungumzo ambapo kuna taarifa tunataka watuletee kimaandishi ili kutoa maamuzi na leo ndio mwisho wa mda tuliokubaliana na  tutatoa maamuzi yatakayowasaidia wote wakiwemo umoja wa madereva teksi (TODA),” amesema mkurugenzi

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted