Saratani ya mlango wa kizazi yaendelea kuwa tishio kwa nchi za Afrika.

Waziri Ummy amesema, miongoni mwa hatua ambazo zimechukuliwa kukabili ugonjwa huo, Serikali imeiomba jumuiya ya kimataifa kushiriki katika mapambano ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

0

Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema, ugonjwa wa saratani umeua watu 25,000 mwaka 2020 na kuufanya ugonjwa huo kuwa tishio zaidi ya Uviko-19 ilioua watu chini ya 1,000 hapa nchini.

Waziri Ummy amesema, miongoni mwa hatua ambazo zimechukuliwa kukabili ugonjwa huo, Serikali imeiomba jumuiya ya kimataifa kushiriki katika mapambano ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Waziri Ummy ameyasema hayo jana  Septemba 26, 2022 jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Taasisi ya The Lancert Oncology ya hali ya  Ugonjwa  wa saratani katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa upande wa Afrika Mashariki.

Alisema jumuiya ya kimataifa inatoa fedha nyingi kwenye magonjwa ya kuambukiza lakini magonjwa yasiyo ya kuambukiza michango ya kudhibiti haitolewi.

“Nimetoa ombi kwa jumuiya ya kimataifa kwa sababu sawa tuna mipango tunataka kutekeleza lakini kama hatuna rasilimali hatuwezi kufika vijijini, kwa hiyo kilio chetu kikubwa ni kuililia jumuiya ya kimataifa ituunge mkono kwenye magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza,” amesema.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaweka mzigo mkubwa kwenye sekta ya afya na tayari serikali ina mipango mizuri ya kukabiliana na saratani lakini changamoto kubwa ni rasilimali fedha.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amekiri kuwepo kwa uhaba wa vifaa tiba na dawa kwa wagonjwa wa saratani na kisukari.

“Watu wanaumwa kisukari, wanaumwa saratani, wanakosa huduma kwa sababu dawa hizi ni kubwa, pia kwa kutambua tuna kiwango kikubwa cha maambukizi ya ini  kama asilimia tano na Ukimwi asilimia 4.7, homa ya ini tunaweza kuambukiza kwa kupena mikono.

“Tumeona ipo haja ya mpango wetu wa taifa wa kupambana na Ukimwi tuupe jukumu la kuwa mpango wa kupambana na Ukimwi, homa ya ini na magonjwa ya ngono,” amesema.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Allphoncina Nanai amesema ugonjwa wa saratani kwa mwaka 2020 ulisababisha vifo vya watu milioni 10.

Ametaja saratani za mapafu, matiti, utumbo mdogo na mkubwa kuwa hatari zaidi huku saratani ya mlango wa kizazi ikiendelea kuwa tishio kwa nchi za Afrika.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted