Liberia yakamata dola milioni 100 za cocaine

Mamlaka ya Liberia yakamata dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya dola milioni 100, kwa msaada wa shirika la kimataifa la dawa za kulevya la Marekani

0

Mamlaka ya Liberia siku ya Jumatatu tarehe 3 Oktoba, ilisema imekamata dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya dola milioni 100, kwa msaada wa shirika la kimataifa la dawa za kulevya la Marekani.

Waziri wa sheria wa Liberia Musa Dean amewaambia waandishi wa habari kuwa shirika la kitaifa la kupambana na dawa za kulevya, kwa msaada kutoka Ofisi ya Kimataifa ya Narcotics na Masuala ya Utekelezaji wa Sheria, amefanya ukamataji huo Jumamosi katika kijiji cha Topoe, kitongoji cha magharibi mwa mji mkuu Monrovia.

Operesheni hiyo ilisababisha “kukamatwa kwa cocaine safi yenye thamani ya dola milioni 100”, alisema.

Raia wa Guinea-Bissau na mshukiwa kutoka Lebanon walikamatwa, aliongeza.

Shirika hilo la dawa halikuweza kuthibitisha ripoti zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba dawa hiyo ilikuwa imehifadhiwa kwenye vyombo vya samaki vilivyohifadhiwa. Ilisema uchunguzi unaendelea.

Mkuu wa idara ya utekelezaji wa dawa za kulevya Marcus Zehyoue amesema “uchunguzi kamili” unaendelea pamoja na msako wa washirika waliotoroka kukamatwa.

Ubalozi wa Marekani nchini Liberia umeipongeza mamlaka ya Liberia kwa kubaini dawa hizo za kulevya, ukisema katika taarifa yake kwamba ni matokeo ya hatua za pamoja za haraka.

“Mafanikio ya operesheni hii ni matokeo ya moja kwa moja ya mawasiliano bora kati ya mashirika ya kutekeleza sheria duniani kote, ikiwa ni pamoja na Brazil, Marekani, na Liberia, miongoni mwa zingine.” iliongeza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted