Dk Mpango: Mradi wa SGR utaongeza ufanisi matumizi ya ukanda huru wa biashara Afrika.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amesema kutekelezwa kwa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza mkoani Kigoma nchini humo hadi Kindu Jamhuri ya Kidemokrasia...

0

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amesema kutekelezwa kwa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza mkoani Kigoma nchini humo hadi Kindu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Gitega nchini Burundi kutaongeza ufanisi katika matumizi ya Ukanda huru wa biashara Barani Afrika kwa kuimarisha usafirishaji wa watu na bidhaa.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akiongoza majadiliano na wawekezaji kuhusu mradi wa reli hiyo ya kisasa, majadiliano yaliofanyika katika Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika linalofanyika Jijini Abidjan nchini Ivory Coast.

Amesema serikali zote tatu zimeweka nia ya dhati ya kutekeleza mradi huo ambapo kwa upande wa Tanzania tayari imekwisha tekeleza miradi unganishi ya reli ya kisasa inayochagiza uwepo wa mradi huo muhimu.

Aidha Makamu wa Rais amesema asilimia 50 ya mizigo inayotoka katika bandari za Tanzania hupelekwa nchi za Burundi na Kongo hivyo uhitaji wa reli hiyo ya kisasa ni muhimu kwa sasa. Amesema uwepo wa idadi watu inayokadiriwa kufikia milioni 170 katika mataifa ya Tanzania, Kongo na Burundi ni uhakika wa soko kwa bidhaa mbalimbali zitakazosafirishwa kupitia reli hiyo.

Pia Makamu wa Rais ameongeza kwamba mradi huo utaokoa gharama kubwa zinazotumika katika kukarabati miundombinu ya barabara inayotumika katika usafirishaji wa bidhaa kutoka bandari zilizopo nchini Tanzania kuelekea mataifa ya Burundi na Kongo.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametaja mradi huo kama njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira kutokana na kutumia nishati ya umeme pamoja na kuimarisha sekta ya kilimo na bidhaa zake katika ukanda uliojaaliwa ardhi yenye rutuba na rasilimali watu ya kutosha.

Waziri wa Miundombinu wa Burundi Dukundane Dieudonneè amesema taifa hilo limekuwa likipoteza zaidi ya dola za marekani milioni 17 kila mwaka katika usafirishaji wa mizigo hivyo mradi huo utasaidia katika kubaliana na hali hiyo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted