Donald Trump Kufika Mahakamani Jumanne

Ameratibiwa  kufika mahakamani kuhusiana na tuhuma na  kashfa ya kumlipa pesa mcheza filamu za ngono kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016.

0

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameeleka New-York, akitokea maeneo anakoishi jimbo la florida ambako Ameratibiwa  kufika mahakamani kuhusiana na tuhuma na  kashfa ya kumlipa pesa mcheza filamu za ngono kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016.

Hali ya usalama imeimarishwa vilivyo  katika eneo la Manhattan, Mali ambako mahakama atakayewasilihswa Trump inapatikana. Trump ni rais wa zamani wa kwanza wa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu, na atafikishwa mahakamani, kuchukuliwa alama za vidole na vile vile  kupigwa picha katika mahakama hiyo kesho Jumanne.

Mawakili Donald Trump tayari wamesema Mteja wao atakanusha mashataka yote anayokabiliana nayo. Mashtaka haswa yanayomkabili yaliyoorodheswa katika maamuzi ya baraza la juu la mahakama lililoidhinisha kushtakiwa kwake, bado hayajawekwa wazi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted