Rais Ruto Athibitisha Kenya Itawania Kuandaa AFCON 2027

Rais wa kenya William Ruto amethibitisha msimamo wa Kenya wa kuwania kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2 (AFCON) 2027

0

Rais wa kenya William Ruto amethibitisha msimamo wa Kenya wa kuwania kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2 (AFCON) 2027

Ruto alikuwa akizungumza baada ya kutazama mechi ya kuburudisha, mashemeji derby iliyozikutanisha Gor Mahia na AFC Leopards katika uwanja wa taifa wa Nyayo ambapo Ingwe iliichapa kogalo 2-1. Rais aliwapongeza kwa mchezo wa kusisimua, kukabidhi kila timu shilingi milioni 1

“Nataka niweke wazi kwa wote kwamba tutabadilisha mchezo huu (mpira), nimefanya mazungumzo na Mhe. Ababu Namwamba na sote tumekubaliana kwamba tutarudisha hadhi ya Kenya katika michezo na soka pale ilipokuwa na inapaswa kuwa.” Aliongeza ruto

Akizungumzia mpango wa kuandaa AFCON 2027, Ruto alitaja kwamba Kenya itawasilisha ombi lao la mwisho Jumatano na kutoa wito kwa mashabiki na wachezaji kutekeleza jukumu lao katika kufanikisha michezo na mashindano.

“Tukishafanikiwa kuleta michezo hapa, ninyi (wachezaji) lazima mhakikishe tunashinda. Tumezungumza pia jinsi viwanja vyetu vimekuwa tupu. Ni ombi langu kwa mashabiki wetu kuepuka kusababisha matatizo wakati wa mechi na kuzingatia nidhamu. Tunataka kufanya viwanja kuwa sehemu nzuri ambapo kila mtu wakiwemo akina mama na watoto wanaweza kuja kufurahia michezo.” Alihitimisha.

Baraza la Mawaziri lilikuwa Desemba 6 2022 liliidhinisha pendekezo kutoka kwa Wizara ya Michezo kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika la 2027.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted