Jaribu wengine sio mimi! Uhuru awakashifu wanasiasa

Kiongozi huyo wa chama hicho alisema kuwa Jubilee itasalia imara na kuungana kuwa kitu kimoja

0
Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta

Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta amekashifu wanasiasa kuhusu jaribio la hivi majuzi la ‘kuteka nyara’ Chama cha Jubilee.

Akizungumza siku ya Jumatatu wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe wa Jubilee katika uwanja wa Ngong Racecourse, Uhuru alisema kuwa hatatikiswa na vitisho.

“Kuna wale ambao wanadhani kazi ni ya vitisho. Lakini sasa wajaribu mwingine, sio mimi,” alisema.

Aidha Uhuru aliwaambia wajumbe kuwa mawazo yake yalimwambia angejiuzulu kutoka kwa chama kama kiongozi wa chama.
“Mawazo yangu yalikuwa yameniambia nipumzike kwenye siasa na kwenda kuhudhuria majukumu mengine. Nilifikiri kwamba leo kwenye mkutano huu ningejiuzulu nikasema muda wangu umekwisha nichague viongozi wengine,” alisema.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa chama hicho alisema kuwa Jubilee itasalia imara na kuungana kuwa kitu kimoja.

Mnamo Februari mwaka huu, Uhuru alithibitisha msimamo wake katika Muungano wa Azimio La Umoja.

Alithibitisha kuwa yeye bado ni mwanachama wa Azimio La Umoja One Kenya, licha ya kimya chake.
“Kustahafu sio kuchoka… ata wengine wanastaafu na nguvu zinaongezeka. Ata kama nimewacha siasa active, mimi bado ni mfuasi wa baba..akiniambia twende lazima twende,” Uhuru alisema.
Aliongeza, “Ingawa nimestaafu siasa, bado ni mfuasi wa Raila. Akiniuliza twende lazima tufanye hivyo. Nilimuunga mkono na nitaendelea kufanya hivyo kwa sababu naamini ni mkweli,” Uhuru alisema.


Rais huyo Mstaafu pia alithibitisha kumuunga mkono kinara wa Upinzani Raila Odinga.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted