TLS  yatia mguu sakata la Bandari

Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) limeunda kamati maalum ya wataalamu kuchambua makubalino yaliyoainishwa katika mkataba wa uendeshaji bandari ya Dar es Salaam kati ya...

0

Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) limeunda kamati maalum ya wataalamu kuchambua makubalino yaliyoainishwa katika mkataba wa uendeshaji bandari ya Dar es Salaam kati ya serikali ya Tanzania na Kampuni ya Dubai ya DP World. 

Rais wa TLS, Wakili Harold Sungusia amesema kamati hiyo itaongozwa na Makamu wa Rais wa TLS, Wakili Aisha Sinda na itakuwa na wajumbe wengine wanne. 

Sungusia amewataja wajumbe wengine kuwa ni Dk. Hawa Sinare – (Makamu Mwenyekiti), Wakili Mpale Mpoki – (Mjumbe), Wakili Stephen Mwakibolwa – (Mjumbe) na Wakili Mackphason Mshana – Katibu 

“TLS inatambua uwepo wa mijadala inayoendelea nchini kuhusu makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendeshaji wa bandari ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai… Kamati itatoa ripoti yake na mapendekezo yake kwa Baraza la Uongozi tarehe 12/06/2023 ili TLS iweze kutoa maoni na kwa hatua zaidi,” amesema Wakili Sungusia.

Wakati mjadala ukizidi kufukuta kuhusu mkataba huo bunge limesema kuwa Azimio hilo sasa bado liko katika ngazi ya kamati ya pamoja kwa mujibu wa kanuni na mara baada ya kamati kumaliza kazi yake azimio hilo limepangwa kuingia bungeni Juni 10, 2023 kwa ajili ya mjadala na kupitishwa na Bunge.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted