Serikali Ya Kenya Yasafisha Idara Ya Uhamiaji

Ni dhahiri wazi Waziri wa Usalama wa Kitaifa nchini Kenya Prof. Kithure Kindiki ana azima ya kuleta mabadiliko makubwa katika idara ya uhamiaji iliyopo jumba la Nyayo Jijini...

0

Ni dhahiri wazi Waziri wa Usalama wa Kitaifa nchini Kenya Prof. Kithure Kindiki ana azima ya kuleta mabadiliko makubwa katika idara ya uhamiaji iliyopo jumba la Nyayo Jijini Niarobi

Waziri Kindiki amekuwa akifanya ziara za kushtukiza katika ofisi za idara hiyo. Lengo ni kuhakikisa mapungufu yaliyopo katika utoaji wa pasipoti yanaangaziwa na mianya ya ufisadi kuzibwa.

Wakenya pamoja na Raia wengine wanao tafuta pasipoti wamekuwa wakilalamikia hulka ya maombi yao ya pasipoti kukawia kupita kiasi.

Siku Ya ijumaa, Kindiki kwa mara nyingine alizuru jumba la Nyayo na kukutana na maafisa waandamizi wa idara ya uhamiaji.

Mkutano huo ulidhamiria kufanya utekelezaji wa mabadiliko ya utendakazi na sera yaliyowekwa ili kutatua suala la ukawiaji katika utoaji wa pasipoti.

“Makataa ya siku 10 ya kumaliza mrundiko wa zaidi ya maombi ya pasipoti 40,000 yangalipo. Ufanyaji kazi kwa zamu usiku na mchana ili kuwezesha uchapishaji kikamilifu wa pasipoti, ununuaji wa mashine ya kisasa ya uchapishaji na kuajiri maafisa zaidi wa uhamiaji vitasaidia kusuluhisha changamoto za kimfumo ambazo zimekuwa zikiathiri utoaji huduma,” alisema Kindiki wakati wa mkutano huo

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted