Tsegay wa Ethiopia Avunja Rekodi Ya Dunia Ya Faith Kipyegon Katika Mbio Za Mita 5000

Bingwa wa Dunia wa mbio za mita 10,000 Gudaf Tsegay amevunja rekodi ya dunia ya mita 5000 iliyowekwa na Faith Kipyegon kwenye  mbio za Diamond League iliofanyika Jimbo...

0

Bingwa wa Dunia wa mbio za mita 10,000 Gudaf Tsegay amevunja rekodi ya dunia ya mita 5000 iliyowekwa na Faith Kipyegon kwenye  mbio za Diamond League iliofanyika Jimbo La Oregon , Marekani.

Mwanariadha huyo wa mbio ndefu wa Ethiopia alitumia dakika 14:00.21 na kukata utepe mbele ya Beatrice Chebet wa Kenya aliyetumia Muda Bora wa Kibinafsi wa dakika 14:05.92. Tsegay bila wasiwasi alimaliza rekodi ya dunia ya Kipyegon ambayo ilikuwa saa 14:05.20. Kipyegon aliweka Rekodi hiyo katika mbio hizo hizo za diamond league nchini Ufaransa Mwezi Juni Mwaka huu.

Katika Mbio za Mita 800, Mkenya Emmanuel Wanyonyi alitwaa ushindi baada ya kumpiku Marco Arop wa Canada.

Bingwa wa Michezo ya Jumuiya ya Madola mita 100 Ferdinand Omanyala alimaliza msimu wake kwa kumaliza katika nafasi ya tatu katika fainali ya Diamond league Oregon, Marekani.

Christian Coleman wa marekani alitwaa ushindi baada ya kumaliza wa kwanza kwa sekunde 9.83.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted