Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania anayedaiwa kuimba uchochezi afikishwa mahakamani.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Sifa Boniventure(25) na Producer wake Ezekia George wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.

0

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Sifa Boniventure(25) na Producer wake Ezekia George wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Wawili hao walikamatwa Septemba 13 kufuatia wimbo wao unaojulikana kama “Tanzania Inaelekea Wapi” wimbo ambao jeshi la Polisi linadai kuwa una maudhui ya kichochezi dhidi ya Serikali.

Kufikishwa kwao Mahakamani ni kufuatia mawakili wanaowawakilisha kupeleka ombi Mahakamani kulitaka Jeshi la Polisi liwapeleke Mahakamani watuhumiwa hao baada ya kunyimwa dhamana.

Sifa na mwenzake wamekaa mahabusu ya polisi kwa takribani siku 6 ambapo ni kinyume cha sheria inayotaka kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ndani ya saa24.

Nchini Tanzania sheria imeweka uhuru wa kuzungumza lakini uhuru huo unaonekana kubanwa na mamlaka ambayo inaonekana kugadhabika na wakosoaji.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted